Pata taarifa kuu
Guinea-Senegal

Rais wa Guinea azishutumu Sengal na Gambia kuhusika katika jaribio la kummalizia maisha

Rais wa Guinea Alpha Conde amezishutumu nchi za Senegali na Gambia kuhusika moja kw amoja katika jaribio la kummalizia maisha la Julay 19 iliopita nchini mwake. Alpha conde ameyasema hayo katika mahojiano na Gazeti mojawapo nchini Senegal la l'enquete pamoja na radio Sud FM. Thuma hizo zimetupiliwa mbali na msemaji kwenye ikulu ya rais wa Senegal. Upande wake Gambia haijatamko lolote kuhusu tuhuma hizo.

l'express
Matangazo ya kibiashara

Majina ya watuhumiwa wa jaribio hilo wote wanaeshi ugenini na hawaja tamka lolote, watu wao wa karibu jijini Conakry wamesema tuhuma hizo hazina msingi wowote.

Alpha Conde alimtaja pia Bah Oury namba 2 wa chama cha upinzani cha UFDG CHA cellou Dalein Diallo, Tibou Camara, waziri wa taifa wa zamani ambae pia alikuwa katibu mkuu kwenye ikulu ya rais katika utawala wa kipindi cha mpito, pamoja pia na mfanyabiashra mashuhuri Amadou Oury maharufu”Sadaka” kutokana na ukarimu wake kwa wananchi wa Guinea.

Rais wa Guibea anawatuhumu ndugu zake hao kwa kosa la kuhusika katika upangiliaji wa jaribio lililo lenga kummalizia maisha katika usiku wa Julay 18 kuamkia Julay 19 iliopita. Katika mahojiano na kituo binafsi nchini Senegal Sud FM. Alpha Conde amethibitisha kwamba shambulizi hilo liliandaliwa kwenye hoteli Merien jijini Dakar kwa mchango wa Senegal na Gambia.

Alpha Conde amesema kutokana na ushahidi alionao, alimtahadharisha Madicke Niang, waziri wa mambo ya nje wa Sengal na mweziwe wa Gambia kwamba shambulizi hilo liliandaliwa katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, ili kukazia shutma hizo amesema kulikuwa na misafara ya nenda rudi kati ya Dakar na Banjul.

Kuhusiana na misafara hiyo kati ya Dakar na Senegal mtu wa karibu wa waziri wa zamani wa taifa katika utawala wa mpito Tibou Camara amesema haishangazi yeyote kwani kama inavyojulikana waziri huyo wa zamani anakwenda Banjul kumuona shemeji yake ambae ni mkewe rais wa nchi hiyo.

Viongozi nchini Senegal wamekanisha tuhuma hizio za kuhusika kwa njia moja ama nyingine za kuvuruga usalama nchini Guinea.

“Hatuwezi kamwe kujihusisha kwa nji amoja ama nyingine katika harakati za kuyumbisha usalama nchini Guinea, Senegal kuna raia milioni mbili wa Guinea huku laki tatu ya raia wa Snegal wanaeshi nchini Guinea” amethibitisha hayo msemaji wa ikulu ya rais wa Senegal Serigne Mbacké Ndiaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.