Sudan-Sudanu kusini - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 30 desemba 2011 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 30 desemba 2011

Watu 17 wauawa katika mashambulizi ya anga mpakani mwa Sudani na Sudani Kusini

Eneo la Sudani kusini
Eneo la Sudani kusini

Na RFI

Watu kumi na saba wamepoteza maisha kusini mwa nchi ya Sudan mpakani mwa nchi hiyo na Sudan Kusini kufuatia shambulio la anga lililofanywa na majeshi ya Sudan.

Msemaji wa wa majeshi ya Sudan Kusini Philip Aguer, amesema kuwa serikali ya Khartoum imeendelea kupeleka vikosi vyake mpakani mwa nchi hizo mbili kwenye maeneo yenye mgogoro na kwamba imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya raia.

Kufuatia tuhuma hizo za Sudan Kusini, serikali ya khartoom kupitia msemaji wa jeshi la nchi hiyo Al Sawarmi Khalid amekanusha majeshi ya nchi hiyo kufanya mashambulizi yoyote siku ya alhamisi yaliyolenga raia wa kusini badala yake amesema kuwa jeshi lake limebaini kuwa wapiganaji zaidi ya 350 wanaopigana vita katika jimbo la darfur wameingia sudan kusini kupitia mpaka huo.

Mashambulizi hayo yameendelea kuzusha hali ya sintofahamu kuhusu uhusiano kati ya nchi hizi mbili ambazo zimekuwa zikigombea eneo la mpaka wa abyei ambako hivi sasa vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani vimepelekwa.

tags: Sudani - Sudani Kusini
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close