Pata taarifa kuu
Sudani

Kundi la waasi la JEM lawashikilia wafanyakazi 49 wa mashirika ya kimataifa

Kundi la waasi wa jimbo la Darfur nchini Sudan la The justice and Equality Movement JEM limetangaza kuwashikilia wafanyakazi 49 wamashirika ya kimataifa pamoja na maofisa wawili wa usalama wa taifa wa Sudan.

Kundi la waasi wa Sudani
Kundi la waasi wa Sudani AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za kukamatwa kwa wafanyakazi hao wa mashirika ya umoja wa mataifa zimethibitishwa na mmoja wa wasemaji wa kundi hilo Bilal Said ambaye amesema kuwa wafanyakazi hao waliingia bila taarifa kwenye eneo ambalo wanalishikilia.

Msemaji huyo amethibitisha kundi lake kuwakamata wafanyakazi hao bila kueleza ni wapi hasa ambako liliwakamata ingawa amesema kuwa wafanyakazi hao na mali zao wako salama.

Kundi hilo limeongeza kuwa hivi sasa linawahoji kuhusiana na kuingia kwenye eneo lao bila taarifa huku wakijua fika kuwa kundi hilo linamgogoro na serikali na kwamba hawaruhusu wafanyakazi wa kimataifa kuingia bila kibali chao.

Msemaji wa majeshi ya UNAMID ya nchini Sudana ameshindwa kuthibitisha taarifa hizo ingawa amekiri kuwa wamepoteza mawasiliano na wafanyakazi 46 raia wa senegal na wenginr toka nchi za Rwanda, Yemen na Ghana.

Kukamatwa kwa wafanyakazi hao kuemkuja ikiwa yamepita majuma kadhaa toka kundi hilo liwateke nyara wafanyakazi 49 raia wa China na baadae kuwaachilia huru, wafanyakazi hao walikuwa wanajenga barabara kwenye jimbo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.