Viongozi wa kijeshi nchini Mali watangaza katiba mpya

Uongozi wa kijeshi nchini Mali umetangaza kuunda katiba mpya na kupanga muhula wa mpito. Katika kipindi hiki ambacho hakikutajwa muda wake baraza la mapinduzi la CNRDRE ndicho chombo kikuu madarakani. Hata hivyo viongozi wa baraza hilo la mapinduzi hawatoruhusiwa baade kugombea madaraka. Wakati huohuo Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi ECOWAS imetangaza kuwatuma viongozi wa nchi sita zinazounda Jumuiya hiyo jijini Bamako kwa lengo la kuwashawishi viongozi wa kijeshi waliendesha mapinduzi kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Serikali hiyo ya kijeshi imetangaza pia kuondowa amri ya kutotoka nje usiku na kufunguwa mipaka yake.
Ishara ya dharau dhidi ya matumaini ya jamii ya kimataifa na kukataliwa na sehemu kubwa ya wanasiasa wa Mali ? Ni kuonyesha Ubabe kabla ya kuwasili kwa ujumbe wa Wakuu wa Nchi za ECOWAS, Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi? Licha ya nia walioendesha mapinduzi ya, serikali hiyo ya Rais Amadou Toumani Toure Machi 22, wanatekeleza vitendo.
Jana jumanne usiku mida ya saa nne kwenye kituo cha televisheni ya taifa matangazo ya ngoma za jadi, yalikatishwa ghafla, watu kumi, wanane waliovalia sare za jeshi na wawili walivalia nguo za raia, na kuzungumza kwa muda wa zaidi ya saa moja wakiwasilisha katiba mpya ya mpito.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya