LIBYA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 22 mei 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 22 mei 2012

Mlipuaji wa ndege ya Lokerbie azikwa nchini Libya

abdelbaset al-megrahi wakati akiugua kansa kabla ya kifo kumkuta
CNN.com

Na Victor Robert Wile

Abdel ali Mohmet al Megrahi, mtu pekee aliyehukumiwa kifungo baada ya kuhusika katika tukio la shambulio la bomu mwaka 1988 katika anga la mjini Lockerbie nchini Scotland amezikwa karibu na mji wa Tripoli nchini Libya.

Mazishi hayo yalifanyika kimya kimya tofauti na shamrashamra alizozipokea kutoka kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Marehemu Kanali Moamar Gadafi ambaye alimkaribisha Megrahi aliporejea kutoka kifungoni Scotland baada ya kutumikia kifungo cha miaka nane kabla ya kuachwa huru.

Mazishi hayo yameelezwa kutohudhuriwa na maafisa wa Serikali na wala hakukuwa na wawakilishi kutoka katika Baraza la Mpito la nchi hiyo.

Megrahi amefariki miaka 11 baada ya kuhukumiwa kwa makosa ya kuhusika na tukio la kulipua ndege katika anga la Uskoti mjini Lockerbie mwezi tarehe 21 Disemba, mwaka 1988 na kusababisha watu 259 kupoteza maisha.

tags: Baraza la Mpito la Waasi Nchini Libya NTC - Libya - Muammar Gaddafi
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close