MALI - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumatano 23 mei 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 23 mei 2012

Serikali ya mpito Mali sasa katika wasiwasi wa kufikia malengo

Waandamanaji wakiwa wametinga katika Ikulu ya Mali, Mei 21 mwaka huu
REUTERS/Adama Diarra

Na Victor Robert Wile

Mchakato wa mwaka mmoja wa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia nchini Mali umeanza kwa dosari jana kufuatia kuwapo kwa hali ya wasiwasi kuwa Mchakato huo huenda usifikie malengo yake.

Wasiwasi huo unakuja baada ya Rais wa Mpito nchini humo Dioncunda Traore kushambuliwa na waandamanaji.

Wapatanishi toka Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Magharibi, ECOWAS wametishia kuwawekea vikwazo wale waliohusika na shambulio dhidi ya Rais huyo hali inayooelezwa kuwa imeteteresha mpango wa makubaliano yaliyofikiwa.

Mkuu wa tume ya ECOWAS, Kdre Desire Ouedraogo amesema tume itafanya uchunguzi kuwabaini waliomshambulia Traore na kuwawekea vikwazo na kuwachukulia hatua.

Shambulio lililotekelezwa limekemewa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Bunge la Mali, wote wakitaka Mamlaka kuhakikishia usalama maafisa wa Serikali ya Mpito.

Shambulio hilo dhidi ya rais wa mpito nchini Mali limelaaniwa na jumuiya kimaitaifa, ECOWAS na kapteni Sanogo ambaye aliongoza mapinduzi dhidi ya serikali kabla ya kuingia katika uongozi wa mpito unaolenga kuirejesha nchi katika utawala wa kikatiba na demokrasia.

tags: Amadou Haya Sanogo - Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS - Mali - Siasa
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close