KENYA-UGANDA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 14 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumatano 15 agosti 2012

Wawili wafa huku wanane wakiokolewa katika mkasa waajali ya ndege za Uganda

Ajali ya ndege ya kijeshi ya Uganda

Na Victor Melkizedeck Abuso

Maafisa wanane wa  kiufundi wa Uganda waliokuwa katika ndege moja ya kivita iliyopotelea katika angaa la Kenya ikienda Somalia wameokolewa wakiwa hai.

Simon Gitau afisaa wa uokoaji kutoka katika shirika la wanyapori nchini Kenya amesema kuwa watu hao waliokolewa kutokana na ndege yao kutoshika moto baada ya kuanguka huku wakipata maiti ya wanajeshi wawili kutoka kwa ndege nyingine iliyoanguka na kushika moto.

Awali,msemaji wa jeshi la Kenya Bogita Ongeri alisema ndege mbili zilikuwa zimepatikana zikiwa zimeungua ila watu waliokuwemo ndani wanaokadiriwa kuwa kumi  hatima yao ilikuwa bado haijafahamika.

Ndege zingine mbili ambazo pia zilianguka katika mlima huo zilipatikana jana na watu saba walikuwa katika ndege hiyo waliokolewa wakiwa hai.

Ndege hizo za kivita zilizonunuliwa nchini Urusi zilikuwa zinakwenda Somalia katika eneo la Kismayo kupambana na wanagamabo wa Al-Shabab mwezi huu wa nane.

AMISOM imekuwa ina wanajeshi elfu 17 wakiwemo kutoka Uganda ambao wanakabiliana na kundi la Al-Shabab.

tags: Kenya - Somalia - Uganda
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close