DRC - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 14 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 14 agosti 2012

Wakuu wa Majeshi wa Mataifa ya Maziwa Makuu kukutana Goma kuhusu M 23

Waasi wa M23

Wakuu wa majeshi kutoka mataifa 11 ya Maziwa Makuu wanakutaka siku ya Jumatano kumalizia mikakati ya kuunda jeshi la pamoja litakalokwenda Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na waasi wa M23 na makundi mengine ya waasi.

Viongozi hao watakutana katika mji wa Goma baada ya makubaliano ya marais wa mataifa hayo waliokutana jijini Kampala Uganda wiki iliyopita kujadili namna ya kukabiliana na waasi wa M 23.

Hata hivyo, changamoto inayokabili wakuu hao wa majeshi ni ikiwa wanajeshi wa Rwanda watajumuishwa katika kikosi hicho baada ya Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo kuituhumu serikali ya Kigali kwa kuwafadhili waasi hao.

Marais wa jumuiya ya mataifa ya Maziwa Makuu watakutana baada ya wiki tatu zijazo kuthathmini mapendekezo yatakayokuwa yamekubaliwa na viongozi wa majeshi ya mataifa hayo.

Baadhi ya Mataifa ya Jumuiya Kimataifa kama Marekani na Uholanzi yamechukua hatua ya kukatiza msaada wa kifedha kwa Rwanda ambayo imepinga hatua.

 

MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close