Wachimba migodi zaidi ya 60 wazikwa hai DRC

Zaidi ya watu 60 wamefariki dunia wiki hii katika mdogi wa madini Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zilizotolewa na redio Okapi ya Umoja wa Mataifa, imeripoti kuwa mauji hayo yalitokea siku ya Jumatatu katika eneo la Pangoy Kilomita 120 kutoka mji wa Manbasa.
Inaelezwa kuwa wachimba madini hao wahawakuwa halali wakati mdogi waliokuwa wanachimba madini kuporomoka na kuwazika wakiwa hai.
Mauji ya wachimba migodi hao pia yamethibitishwa na serikali za mitaa ambayo pia imesema mdogi huo haukuwa unatambuliwa kisheria kutokana na mapigano kati ya waasi na wanajeshi na baadaye kupigwa marufuku kwa mdogi huo.
Haijafahamika hasa ni madini gani yaliyokuwa yanachimbwa katika mgodi huo huku ajali nyingi zikiendelea kushuhudiwa katika migodi mbali Mashariki mwa nchi hiyo.
Mashariki mwa DRC kuna utajiri mkubwa wa madini mbalimbali kama dhahabu.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya