Afrika Kusini-Zimbabwe - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 24 agosti 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 24 agosti 2012

Rais Zuma atakiwa kujiuzulu, Marekani yakemea uvamizi wa ofisi za wanaotetea ushoga nchini Zimbabwe

Rais Jacob Zuma anayetakiwa kujiuzulu kutokana na vurugu kwenye migodi
REUTERS/Siphiwe Sibeko

Na Victor Robert Wile

Ibada maalumu ya mazishi ya wafanyakazi 44 wa mgodi wa Platinum waliouawa na polisi nchini Afrika kusini imefanyika hapo jana huku serikali ya rais jackob Zuma ikiahidi kupata ukweli wa mauaji hayo.

 

Rais Zuma hakuhudhuria ibada hiyo ingawa alituma wawakilishi wake na kuahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio huku baadhi ya wananchi wakionesha kuchukizwa kwa rais kushindwa kufika wakati wa mazishi hayo.

Julius Malema aliyesimamaishwa uanachama wa chama cha ANC ameshutumu serikali kwa kutekeleza mauji hayo na kumtaka rais Zuma kuwajibika kwa kujiuzulu.
Wakati huohuo Serikali ya Marekani imelaani vikali tukio la uvamizi wa ofisi za

Wakati huohuo wanaharakati wanaotetea ushoga nchini Zimbabwe na kuongeza kuwa tukio hilo ni kinyume na sheria za haki za binadamu na niudhalilishaji.

Jumatatu ya wiki hii polisi nchini humo walivamia ofisi za wanaharakati hao na kuchukua kopyuta pamoja na nyaraka nyingine muhimu katika tukio ambalo watu kadhaa walijeruhiwa.

Polisi nchini Zimbabwe inawashikilia watu 44 ambao wanajihusisha na ndoa za jinsia moja kwa tuhuma ya kwamba wanashikilia nyaraka za siri ambazo zinahatarisha usalama wa nchi hiyo.

tags: Afrika Kusini - Marekani - Zimbambwe
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close