NIGERIA -
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumamosi 08 septemba 2012 -
Taarifa za ivi karibuni : Jumamosi 08 septemba 2012
7 wauawa katika majibizano ya risasi kati ya jeshi la Nigeria dhidi ya wapiganaji wa Boko haram

Wananchi wa Nigeria wakishuhudia moja ya shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram
Reuters
Mapigano makali yamezuka ijumaa kati ya wapiganaji wa kundi la kiislam la Boko haram dhidi ya majeshi ya serikali ya Nigeria na kusababisha vifo vya watu saba jeshi limethibitisha.
Luteni Kanali Sagir Musa amesema kundi la watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa Boko haram wamefanya mashambulizi katika vituo vya ukaguzi vya jeshi huko Maiduguri ambapo wanajeshi walikuwa katika zoezi la ukaguzi.
Kanali Musa ameongeza kuwa majibizano ya risasi yaliua wapiganaji saba na kukamatwa kwa wengine 13 na hakuna majeruhi kwa upande wa wanajeshi wa serikali.
Kundi la Boko Haram limekuwa likituhumiwa kufanya mashambulizi mbalimbali nchini humo na kusababisha vya zaidi ya watu elfu moja na mia nne tangu mwaka 2010.







MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya