ETHIOPIA-SWEDEN - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Jumanne 11 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Jumanne 11 septemba 2012

Waandishi wa habari wawili raia wa Sweden walioachwa huru nchini Ethiopia, wapumzika kabla ya kurejea nyumbani

waandishi wa habari Johan na Martin
waandishi wa habari Johan na Martin

Na Ali Bilali

Waandishi wa habari wawili raia wa Sweden walioachiwa huru nchini Ethiopia kufuatia msamaha wa rais, wamewekwa sehemu ya siri kabla ya kukutana na familia zao. Waandishi hao wameachwa huru baada ya kuzuiliwa kwa muda wa myezi kumi na minne.

 

Kjell Persson baba wa Johan Persson amesema kwamba mwanae pamoja na mwenzie Martin Schibbye waliondoka jijini Addis Abeba jana usiku na sasa wanapumzika, kabla ya kureja nchini, amethibitisha kuwa alizungumza kwa njia ya simu na mwanaye mapema leo asubuhi, bila hata hivyo kusema alikuwa yupo wapi.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Kjell Persson, Johan na Martin wamekuwa jela kwa muda wa miezi kumi na minne, bila amani na utulivu, hivyo wanahitaji kupumzika, kula, kupata habari kuhusu Sweden na kukutana na dactari kabla ya kureja nyumbani kwao na kukutana na waandishi wa habari na ndugu jamaa na marafiki.

Serikali ya Ethiopia ilitoa msahama na hatimaye kuwaachia waandishi wa habari wawili raia wa Sweden ambao walikamatwa mwaka uliopita na kisha kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi na moja jela kwa kosa la kufadhili ugaidi.

Waandishi hao wawili wa habari walikamatwa kwenye eneo la waasi na kushtakiwa kwa kosa la kusaidia ugaidi katika nchi hiyo lakini msamaha wake uliidhinishwa na Marehemu Waziri Mkuu Meles Zenawi.

 

tags: Ethiopia - Sweden
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close