Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Matokeo ya awali yaonesha kuwa wananchi wa Zimbabwe waunga mkono rasimu ya Katiba Mpya

Matokeo ya awali ya kura ya maoni kuhusu Katiba mpya nchini Zimbabwe yanaonesha kuwa idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wamepiga kura ya ndio kuunda mkono rasimu mpya ya katiba.

Matangazo ya kibiashara

Hesabu iliyofanywa na kundi la Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai inaonesha kuwa zaidi ya asilimia tisini ya wananchi nchini humo wamepiga kura ya ndio na dalili zote zinaonesha kuwa rasimu hiyo imeungwa mkono kikamilifu.

Uwepo wa katiba mpya nchini humo utawezesha kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mpya ambao utaamua ikiwa rais wa sasa Robert Mugabe atawania urais nchini humo au la.

Katiba mpya inaweka muda wa mihula miwili kwa rais kutawala nchi hiyo na inaipa bunge nguvu zaidi ya kuidhinisha uteuzi uliofanywa na rais.

Ikiwa Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 89 atawania tena urais nchini humo ataweka historia kuwa kiongozi mkongwe zaidi barani Afrika kuwania urais.

Rais Mugabe ambaye amekuwa rais tangu mwaka 1980 pia ameunga mkono katiba hiyo mpya, na ikiwa atachaguliwa kwa mihula miwili ataongoza nchi hiyo kwa miaka kumi ijayo.

Mbali na hayo, washirika wanne wa karibu wa Waziri Mkuu Tsvangirai walikamatwa siku ya Jumapili na polisi kwa tuhma za kuwadhihaki polisi.

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na mshauri wa kisiasa wa Tsvangirai Thabani Mpofu na wakili maarufu wa haki za bindamu Beatrice Mtetwa.

Waangalizi wa kutoka muungano wa mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC wamesema zoezi hilo la kura la maoni limefanyika kwa amani licha ya visa vichache vya machafuko.

Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe unatarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.