Pata taarifa kuu
MALI

Umoja wa Ulaya wapongeza uchaguzi wa wabunge nchini Mali

Umoja wa Ulaya umepongeza zoezi la uchaguzi wa wabunge nchini Mali na kusema kuwa uchaguzi huo ni hatua nyingine ya mafanikio kufuatia uchaguzi wa rais uliofanyika kwa amani mnamo mwezi Agosti.

Wananchi wakipiga kura nchini Mali jana Jumapili
Wananchi wakipiga kura nchini Mali jana Jumapili REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa waangalizi wa umoja wa Ulaya EU wamepongeza zoezi hilo leo Jumatatu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi endapo duru la pili litahitajika.

Mkuu wa ujumbe huo Louis Michel amepongeza maandalizi yaliyofanikisha uchaguzi huo,hasa kuhusiana na vifaa vya utnedaji kazi hiyo na hali ya kibinadamu iliyokuwepo wakati wa shughuli za kupiga kura.

Uchaguzi wa jana Jumapili nchini Mali ni ishara ya hatua ya kwanza ya mafanikio kuelekea kujiimarisha baada ya kutumbukia katika machafuko na mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Machi mwaka jana, na inakamilisha mchakato ulioanza kwa uchaguzi wa Rais Ibrahim Boubacar Keita mwezi Agosti.

Hata hivyo wapiga kura walizuiwa kushiriki zoezi hilo na waandamanaji wa Tuareg katika mji wa Kaskazini Mashariki wenye watu wapatao elfu kumi na nne , wakati kulipokuwa na maandamano katika ngome ya waasi hao Kaskazini mwa mji wa Kidal huku kukiwa na ripoti ya kuibiwa kwa sanduku la kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.