Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Mazungumzo ya Sudani Kusini yakwama tena licha ya vitisho vya vikwazo vya Marekani na UN

Wajumbe wa serikali ya Sudan Kusini na wale wa waasi wameshindwa kurejea tena katika meza ya mazungumzo jijini Addis Ababa nchini Ethiopia jana Alhamisi licha ya vitisho vya kuwekewa vikwazo na Marekani na Umoja wa Mataifa. 

Msemaji wa serikali ya Sudani Kusini Ateny Wek Ateny
Msemaji wa serikali ya Sudani Kusini Ateny Wek Ateny www.telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa pande zote mbili wanalaumiana kuhusu kutoanza kwa mazungumzo hayo yanayosimamiwa na muungano wa nchi za Maendeleo za Afrika Mashariki IGAD.

Msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Ateny Wek Ateny amesema serikali ya Juba iko tayari kuendelea na mazungumzo hayo ya amani lakini haitaki kushikirishwa kwa wanasiasa saba wa upinzani walioachiliwa huru.

Waasi wanasema ni lazima wanasiasa hao walioachiliwa huru washiriki katika mazungumzo hayo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.