Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-Usalama

Wakenya wawili waokolewa kutoka mikononi mwa al Shabab

Jeshi la Kenya limefanikiwa kuwaokoa raia Kenya waliyokua walitekwa nyara na tangu mwaka 2011 na wanamgambo wa kislamu wa kundi la al Shabab,imefahamisha wizara ya ulinzi ya Kenya.

Wanajeshi wa Kenya waliyo katika kikosi cha Umoja wa Afrika Kinacholinda Amani nchini Somalia AMISOM.
Wanajeshi wa Kenya waliyo katika kikosi cha Umoja wa Afrika Kinacholinda Amani nchini Somalia AMISOM. AFP / AU-UN IST PHOTO
Matangazo ya kibiashara

 James Kiarie Gichuhi mfanyakazi wa shirika la kihisani la CARE International na Daniel Njuguna Wanyoike, mfanyakazi wa kampuni ya usafirishaji walitekwa nyara walipokua wakiendesha shughuli zao kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka na nchi ya Somalia, amethibitisha msemaji wa wizara ya ulinzi ya Kenya, Willy Wesonga.

Watu hao wameathirika kiakiali kutokana na jinsi wanavyoongea, amesema Wesonga, akibaini kwamba viongozi bado wanajaribu kuthibitisha uraia wao.

Wizara ya ulinzi ya Kenya imebaini kwamba mateka hao wameokolewa na wanajeshi wa Kenya waliyoptumwa nchini Somalia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika Amisom wanaoshirikiana na jeshi la serikali dhidi ya wanamgambo wa kundi la al Shabab, lakini wizara hio imejizuia kutoa taarifa yoyote inayohusiana na operesheni ya kikosi hicho nchini Somalia.

Wesonga amesema kwamba wameokolewa kwenye aridhi ya Somalia, ambako kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika Amisom kimeanzisha operesheni kabambe dhidi ya kundi la al Shabab. Wesonga amebaini kwamba wanajeshi wa Kenya wanaendesha shughuli zao kusini mwa somalia.

Kiongozi wa CARE International amethibitisha kwamba Gichuhi alikua dreva kwenye shirika hilo katika kambi ya Hagadera, karibu na Dadaab kaskazini mwa Kenya, ambayo inawahifadhi wakimbizi 105.000 kutoka Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.