Pata taarifa kuu
ALGERIA-Uchaguzi

Raia wa Algeria wamchagua rais mpya

Wapiga kura nchini Algeria wanaanza zoezi la kupiga kura hii leo kuchagua raisi, huku rais anayemaliza muda wake Abdelazizi Bouteflika akitarajiwa kushinda kwa awamu ya nne.

Moja kati ya vituo vya kupigia kura katika mji mkuu wa Algeria,Alger, ambako wanawake hawa wa Algeria wakipiga kura kumchagua rais mpya
Moja kati ya vituo vya kupigia kura katika mji mkuu wa Algeria,Alger, ambako wanawake hawa wa Algeria wakipiga kura kumchagua rais mpya AFP PHOTO/PATRICK BAZ
Matangazo ya kibiashara

Bouteflika, mwenye umri wa miaka 77, alishika madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 1999 na kuchaguliwa tena mwaka 2004 na 2009 baada ya kufanya mabadiliko ya katiba yaliyomruhusu kugombea tena, anapewa nafasi kubwa nchini humo kutokana na kuchangia kukomesha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1990 yaliyosababisha vifo takribani laki mbili.

Jumla ya wagombea sita wanawania kiti cha uraisi akiwemo mshindani wa karibu wa Bouteflika Ali Benflis, mwenye umri wa miaka 69, wazairi mkuu wa zamani ambaye aliamua kuwania kiti cha uraisi kufuatia kukosekana kwa takribani miaka 10 katika siasa baada ya kupoteza nafasi katika uchaguzi wa mwaka 2004.
Zaidi ya raia milioni 22 wanatazamiwa kupiga kura.

Siku ya leo hakuna kazi na italipwa katika idara na mashirika ya serikali. Raia wengi Algeria wanampigia upato rais Bouteflika, ambaye ameshongoza taifa hilo kwa mihula mnne sasa.

Abdelaziz Bouteflika ameshiriki katika upigaji kura, ambapo mapema asubuhi aliwasili kwenye kituo cha kupigia kura nambari 34 kilitengwa kwenye shule liitwalo Bachir EL ibrahimi katika eneo la Biar linalopatikana kwenye milima ya Alger, huku akizunguukwa na ndugu zake wawili, Saïd, ambae ni mshauri wake maalum pamoja na mtoto wa dada yake.

Mjumbe maalum wa Bouteflika, amesema, rais aliwasili akiwa kwenye kiti cha magurudumu mawili kikisukumwa na watu wake wa karibu, huku akibaini kwamba rais huyo hawezi kusimama.

Rais Bouteflika amekua amevalia suti nyeusi, akitabasamu, huku akiwasabahi waandishi wa habari kwa ishara za mkono kama inavyoonyesha video hii.

  Benfils ametuma waangalizi 60.000 katika vituo mbalimbali vya kupigia kura. Amebaini kwamba iwapo wizi wa kura utadhihirika, basi hatosita kunyooshea kidole.

Vituyo vya kupigia kura vinatazamiwa kufungwa leo jioni kwenye saa mbili usiku saa za Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.