Pata taarifa kuu
SENEGAL-Sheria

Senegal: Karim Wade mbele ya vyombo vya sheria

Vyombo vya sheria nchini Senegal vimeamua kumfikisha mbele ya mahakama Karim Wade. Karim Wade, ambae ni mtoto wa aliekua rais wa Senegal Abdoulaye Wade anatuhumiwa kupata utajiri kinyume cha sheria. Ni mwaka mzima sasa, akiwa katika kifungo cha muda katika jela liitwalo Rebeuss. Duru za kuaminika zinabaini kwamba, mahakama inayomsikiliza Karim Wade ina muda wa miezi miwili wa kuandaa kesi hio.

Karim Wade, mtoto wa aliekua rais wa Senegal Abdoulaye Wade atuhumiwa kupata utajiri kinyume cha sheria.
Karim Wade, mtoto wa aliekua rais wa Senegal Abdoulaye Wade atuhumiwa kupata utajiri kinyume cha sheria. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili Karim Wade ziliendeshwa kwa muda wa miaka miwili, huku akiziwiliwa jela kwa kipindi cha mwaka moja sasa.

Awali, waendesha uchunguzi walitafuta ushahidi kuhusu jumba la kifahari lenye thamani ya karibu Uro milioni moja, na baadae iliongezwa tuhuma nyingine inayomuhusisha kumiliki akaunti zaidi ya ishirini mjini Monaco, nchini Ufaransa.

Uchunguzi huo ndio ulisababisha kifungo cha muda kinaongezwa.
Kwa sasa, chanzo kiliyo karibu na faili hii, wanajua kwamba Karim Wade atafikishwa mbele ya mahakama husika inayopamabana na utajiri usiyo halali miezi miwili ijayo.

Hadi sasa hawajajua ni kiwango gani cha makosa anayotuhumiwa.

Karim Wade à akiwasili ili kusikilizwa kwa mara ya kwanza tuhuma zinazomkabili kwenye mahakama inayopambana dhidi ya utajiri usiyo halali mjini Dakar, machi 15 mwaka 2013.
Karim Wade à akiwasili ili kusikilizwa kwa mara ya kwanza tuhuma zinazomkabili kwenye mahakama inayopambana dhidi ya utajiri usiyo halali mjini Dakar, machi 15 mwaka 2013. AFP/SEYLLOU

Lakini mapema mwanzoni mwa juma hili, alipokua akisikilizwa katika ofisi ya mashitaka, kiongozi wa mashitaka aliomba Karim Wade na watuhumiwa wenzake wafikishwe mbele ya mahakama ili kujieleza kuhusu jumba la kifahari lenye thamani ya Uro milioni 518.

Miongoni mwa watuhumiwa, anafahamika mwanahabari Cheikh Diallo, aliekua mshauri wa Karim Wade, ambae hajatendewa haki na vyombo vya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.