Pata taarifa kuu
ALGERIA-Uchaguzi

Algeria: Ali Benfils aapa kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi

Kumekuwepo jaribio la wananchi wanaounga mkono upinzani nchini Algeria kutaka kuharibu zoezi la uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hapo jana wakati huu taifa hilo likisubiri matokeo ya urais, ambayo huenda yakashuhudia rais mkongwe wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika akishinda muhula wa 4 wa kuliongoza taifa hili.

Watoto wakichezea kadi za uchaguzi mjini Rafour,aprili 17. Mmoja kati ya wapigakura wawili ameshiriki uchaguzi wa rais.
Watoto wakichezea kadi za uchaguzi mjini Rafour,aprili 17. Mmoja kati ya wapigakura wawili ameshiriki uchaguzi wa rais. REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Dakika chache tu baada ya tangazo la waziri wa mambo ya ndani, Ali Benfils anaegombea kiti cha urais katika uchaguzi uliyofanyika jana nchini Algeria, ametangaza kwamba hatokubali matokeo ya uchaguzi , akibaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.

Amesema yuko tayari “ kutumia hoja za kisiasa na utulivu ili kuonyesha kuwa kulikuepo na wizi wa kura”, huku akibaini kwamba “tarehe ya jana itabaki ni kumbukumbu kwake ya uhalifu mkubwa dhidi ya nia na kuwanyima wananchi haki yao”

Licha ya uchaguzi huo kufanyika kwa amani hapo jana zaidi ya watu 70 wameripotiwa kujeruhiwa kufuatia makabiliano kati yao na polisi wakipinga jinsi zoezi la upigaji kura lilivyofanyika kwenye baadhi ya maeneo.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa mchana huu na waziri wa mambo ya ndani wa Algeria, Tayib Belaiz, matokeo ambayo tayari yamesusiwa na kiongozi wa upinzani na mpinzani wa karibu wa rais Bouteflika, Ali Benflis akidai uchaguzi haukuwa huru na haki.

Ali Benfils alitaka kutangaza mewenyewe matokeo yake ya uchaguzi laikini ametahadharishwa na baraza la kikatiba, ambalo ni taasi pekee inayo majukumu ya kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Benfils amepanga kutoa tangazo lingine mchana baada ya kutangaza kwa matokeo. Jana jioni wafuasi wa Abdelaziz Bouteflika waliandamana katika miji mbalimbali ya Algeria, huku wakifyatua fataki na kupiga honi kwa wingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.