Pata taarifa kuu
BURUNDI-Upinzani-Sheria

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi ahojiwa

Mwenyekiti wa muungano wa vyama vya upinzani visivyo na uwakilishi bungeni nchini Burundi ADC-Ikibiri amefikishwa jana mahakamani mjini Bujumbura kujibu mashtaka yaliyowasilishwa na chama tawala cha CNDD -FDD kwa kushirikiana na redio Rema FM ya Burundi.

LEonce Ngendakumana amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yaliyowasilishwa na chama tawala cha CNDD -FDD kwa kushirikiana na redio Rema FM.
LEonce Ngendakumana amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yaliyowasilishwa na chama tawala cha CNDD -FDD kwa kushirikiana na redio Rema FM. AFP PHOTO/JOSE CENDON
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa saa zisizopungua sita, Léonce Ngendakumana amesikilizwa na mwendesha mashtaka kwa kosa la kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kama taarifa kwa kile alichokiita janga la kibinadamu ambalo linaweza kutokea hivi karibuni nchini humo.

Chama tawala cha CNDD -FDD na redio Rema FM inayosadikiwa kuwa karibu na chama hicho vimelalamikia kauli ya kiongozi huyo wa upinza ya kulinganisha kituo hicho cha redio na Radio Mille Collines (RTLM) nchini Rwanda mwaka 1994 kuandaa mauwaji ya kimbari.

Tayari siku ya alhamisi juma lililopita, Ngendakumana amehojiwa kwa madai hayo ambayo kwa mujibu wa msemaji wa chama tawala Onésime Nduwimana hayakubaliki na kwamba ni mabaya.

Kulingana na msemaji huyo, Léonce Ngendakumana atalazimika kutoa ushahidi wake na tayari muendesha mashitaka mjini Bujumbura amempa Ngendakumana makataa hadi tarehe 25 mwezi huu kuwasilisha ushahidi wote wa madai yake.

Hayo yakijiri, waandishi wa habari watatu wa redio mbili zinazojitegemea wamekua wakitafutwa na vyombo vya sheria kwa madai kwamba wamekua wakitoa habari zisiyokua za kweli kwenye vituo vyao vya redio.

Waandishi hao ni pamoja na Alexis Nibasumba muandishi wa habari wa kituo cha redio Bonesha fm mkoani Bururi kusini mwa nchi, Alexis Nkeshimana muandishi wa kituo cha redio Bonesha fm mkoani Bubanza magharibi mwa nchi na Eloge Niyonzima, muandishi wa habari wa kituo cha redio Rpa mkoani Bubanza magharibi mwa Burundi.

Kiongozi huyo wa muungano wa vyama vya upinzani ADC-Ikibiri na waandishi hao wa habari wanasakamwa na ofisi ya mashitaka juma moja tu baada ya taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa kutoa onyo kali kwa serikali ya Burundi ukiituhumu kuwagawiya silaha vijana wa chama tawala Cndd-fdd “Imbonerakure”, tuhuma ambazo serikali ya Burundi ilikanusha na kusema kwamba tuhuma hizo hazina msingi, na kuwatuhumu wapinzani kuzagaza habari za uzushi.

Hivi karibuni serikali ya Burundi ilichukua hatua ya kumfukuza mkuu wa kitengo cha usalama kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (Bnub), Paul Debbie, ikibaini kwamba haina imani naye.

Umoja wa Mataifa ulilani hatua hio ya serikali ya Burundi. Awali Umoja wa Mataifa ulifahamisha kwamba utawachukulia hatua kali hadi kuwafikisha mbele ya mahakama ya kimataifa wale wote watakaohusika na kuchochea vurugu nchini Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.