Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-Shambulio

Waasi wa Sudani Kusini watuhumu kuwaua raia

Waasi wa Sudani Kusini wanaoongozwa na Riek Machar wamekana kuhusika na mauaji ya mamia ya raia katika kijiji kimoja kinachopatiokana katika mji wa Bentiu, na kulituhumu jeshi la serikali na washirika wake kwamba ndio walihusika na mauaji hayo.

Miili ya raia wliyouawa ikitupwa pembezuni mwa barabara mjini Bentiu, Sudani Kusioni, aprili 20 mwaka 2014
Miili ya raia wliyouawa ikitupwa pembezuni mwa barabara mjini Bentiu, Sudani Kusioni, aprili 20 mwaka 2014 REUTERS/Emre Rende
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa mataifa ulituhumu juzi jumatatu waasi wa Riek Machar kuwaua raia kulingana na kabila zao katika mapigano na jeshi la serikali katika mji wa Bentiu.
Kwa mujibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini(Minuss), mauaji yalianza aprili 15, siku ambayo waasi walifahamisha kuuteka mji huo.

Kundi la waasi wa Sudani Kusini limefahamisha katika tangazo liliyotoa kwamba tuhuma hizo hazina msingi, na ni uzushi uliyotengenezwa na maadui wake, kwa lengo la kulipaka tope.

“Jeshi la serikali na washirika wake ndio wanahusika na mauaji ya raia wa Sudani Kusini katika mji wa Bentiu”, amethibitisha Lul Koang, msemaji wa wapiganaji wa kundi la waasi, huku akibaini kwamba serikali walitekeleza mauaji ya kikatili dhidi ya raia wasiyokua na hatia.

Aprili 15, msemaji huyo wa wapiganaji, alifahamisha kwamba wapiganaji wa kundi la waasi walikamilisha operesheni ya kusafisha na kulinda nje na ndani ya mji wa Bentiu.

Siku hiohio takriban raia 200 waliyokimbilia msikitini waliuawa na waasi wa Riek Machar, Umoja wa Mataifa umethibitisha huku ukibaini kwamba raia wengine waliuawa kanisani na hospitalini. Raia hao ni kutoka jamii ya Dinka, umeendelea kusema Umoja waMataifa.

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mauaji ya kikabila dhidi ya raia yaliyofanyika hivi karibuni katika mji wa Bentiu nchini Sudani Kusini na kusababisha mauaji ya mamia ya raia nchini humo. Mamia ya raia waliuawa juma liliyopita katika mji wa Bentiu nchini Sudani Kusini, na wengine walilazimika kuyahama makaazi yao.

Umoja huo wa mataifa umesema kuwa tukio hilo ni baya kuwahi kutokea katika nchi hiyo inayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mapambano baina ya serikali na waasi.

Raia waliyonusurika walikimbilia katika kambi iliyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji wBentiu, lakini kwa sasa kambi hio imezidiwa na idadi ya wakaimbizi, ambayo ni kubwa.

Raia wakiwa katika kambi iliyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Bentiu, januari mwaka 2014.
Raia wakiwa katika kambi iliyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Bentiu, januari mwaka 2014. AFP/SIMON MAINA

Tangu yalipotokea mauaji hayo katika mji wa Bentiu, idadi ya wakimbizi imeongezeka kutoka 8000 hadi 20.000, na hali hio husababisha matatizo makubwa, hususan uhaba wa maji, na imekua shida kuwahudumia kiafya.

Kungineko nchini Sudani Kusini idadi ya wakimbizi wa ndani imekua ikiongezeka siku baada ya siku.

Kwa sasa matawi ya Ofisi ya Umoja yanawapa hifadhi wakimbizi 80.000 kutoka nchi nzima.

Watu wenye silaha kutoka jamii ya Dinka, walishambulia juma liliyopita kambi moja inayopatikana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Bor.

Wengi miongoni mwa wakimbizi wanaopatikana katika kambi hio ni kutoka jamii ya Nuer.

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa walikabiliana na watu hao, lakini wanajeshi wawili wa kikosi hicho waliuawa.

Mkuu wa shughuli za misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini,Toby Lanzer amesema watu wengi waliuawa kikatili juma liliyopita.

“Niliyoshuhudia juma liliyopita ni wazi kwamba watu wengi waliuawa kiakatili, baadhi waliuawa sokoni, karibu na hospitali, kanisani, na sehemu zingine za ibada, ni machafuko mabaya kuwahi kutokea katika mji huo”, amesema Lanzer.

Umoja wa Mataifa umeomba uchunguzi uanzishwe, na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa waliyohusika katika mauwaji yaliyotokea juma liliyopita katika mji wa Bentiu, alikini itakua vigumu, na watu wamekua wakijiuliza itakuaje kwa waasi wa Riek Machar wafanye uchunguzi kwa uhalifu ambao huenda walitekeleza.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umekua na hofu kutokana na wito wa kukuza chuki za kikabila na uhasama ambao umekua ukitolewa na kituo cha redio Bentiu. Hali hio inakumbusha yaliyotokea nchini Rwanda kabla ya mauaji ya halaiki.

Umoja wa Mataifa uliongeza idadi ya wanajeshi tangu yalipoanza machafuko. Kwa sasa idadi ya wanajeshi hao imefikia 8500. Lakini wanajeshi hao hawawezi kuingia katika mapigano,wana majukumu tu ya kulindia usalama matawi ya ofisi ya Umoja wa Mataifa yanayowapa hifadhi wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.