Pata taarifa kuu
DRC-FDLR

Jumuiya ya kimataifa yataka waasi wote wa FDLR kusalimisha silaha zao

Siku mbili zikiwa zimepita toka waasi wa kihutu wa Rwanda wanaopigana mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC wasalimishe silaha zao kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa nchini humo, jumuiya ya kimataifa imetaka wapiganaji wote wa kundi hilo kujisalimisha.

Silaha ambazo zilisalimishwa na waasi wa FDLR, nyuma wanaonekana vijana wa kundi hilo waliojisalimisha
Silaha ambazo zilisalimishwa na waasi wa FDLR, nyuma wanaonekana vijana wa kundi hilo waliojisalimisha MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda na wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda walijisalimisha kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Kanyabayonga.

Reddition de militants du FDLR, à Kateku, dans l'est de la RDC, le 30 mai 2014.
Reddition de militants du FDLR, à Kateku, dans l'est de la RDC, le 30 mai 2014. REUTERS/Kenny Katombe

Saa chache baada ya kujisalimisha, jumuiya ya kimataifa imeendelea kutoa wito kwa wapiganaji wengine wa kundi hilo ambao hawakuwa tayari kujisalimisha siku ya Jumamosi kufanya hivyo kwa mustakabali wa amani ya mashariki mwa DRC.

Waasi wa FDLR walitangaza juma moja lililopita kuwa wako tayari kujisalimisha kwa Umoja wa Mataifa nchini DRC kwa masharti ya kupatiwa hifadhi ya kupewa msamaha ambao sasa utawashuhudia wapiganaji hao wakirudi uraiani.

Baada ya kuwasili kwenye kambi ya Kanyabayonga, wapiganaji hao walipokelewa na maofisa wa MUNUSCO nchini humo ambao walianza kuzipokea silaha walizokuwa nazo wapiganaji hao wa FDLR ambao wamekuwa wakisakwa na vikosi vya Serikali.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, inalituhumu kundi hilo la FDLR kwa kuhusika na mauji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo zaidi ya watutsi laki nane waliuawa kutokana na mapigano haya.

Licha ya kundi hilo kutaka kuwa na mazungumzo na Serikali yao ya Rwanda, utawala wa rais Paul Kagame umesisitiza kuwa kamwe hauwezi kufanya mazungumzo na waasi hao ambao wamehusika na mauaji ya mamilioni ya watu nchini humo.

Kauli ya Rwanda ilisababisha waasi hawa wa FDLR kutangaza kujipanga kwaajili ya kuvamia nchi hiyo kushinikiza Serikali yao kuerejea kwenye meza ya mazungumzo.

Waasi hao sasa baada ya kujisalimisha watakuwa na uamuzi wa kuamua kurudi nchini mwao ama kuomba hifadhi kwenye nchi jirani hii ni kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Askari wa UN wakitazama silaha ambazo zilisalimishwa na waasi wa kundi la FDLR
Askari wa UN wakitazama silaha ambazo zilisalimishwa na waasi wa kundi la FDLR REUTERS/Kenny Katombe

Zaidi ya wapiganaji 105 wa kundi hilo walijisalimisha siku ya Jumamosi wengi wakiwa ni vijana wadogo waliokuwa wakipigana kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Major Jean-Pierre Faustin Mugisha ni mmoja wa makamanda wa kunfi la FDLR yeye anasema amefurahishwa na namna walivyopokelea na maofisa wa umoja wa matuafa “Tuliwasili tukiwa tumechelewa kidogo, tukapokelewa na kuwekwa sehemu ile asubuhi na kisha tukapewa walau kitu cha kunywa, kwakweli tulipokelewa vizuri”. Anasema Major Jean-Pierre Mugisha.

Hatua ya wapiganaji hawa kutangaza kujisalimisha ni muhimu kwenye vita dhidi ya waasi mashariki mwa DRC na sasa kazi ambayo imesalia ni kwa wanajeshi wa Serikali ya DRC, FARDC kuwakabili waasi wa ADF-Nalu wa nchini Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.