ICTR yathibitisha hukumu ya kifungo cha miaka jdela kwa Agustin Bizimungu
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari iliyoko mjini Arusha ICTR, hapo jana imethibitisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda wakati huo, Augustin Bizimungu.
Imechapishwa:
Cheza - 03:00
Jaji aliyekuwa anasikiliza rufaa iliyokatwa na Bizimungu, Jaji Theodor Meron amesema upande wa utetezi haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kuunga mkono rufaa yao na kwamba mahakama imemkuta na hatia ya makosa ya kuchochea mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya watu wa Kitutsi.
Mahakama hiyo pia imemkuta Bizimungu na hatia ya kosa la kutoa hotuba iliyoelekeza kutekelezwa kwa mauaji ya Watutsi siku chache kabla ya yeye kutangazwa kama mkuu wa majehsi ya Rwanda mwaka 1994.
Wachambuzi wa mambo wanaizungumziaje hukumu aliyopewa Bizimungu anayedaiwa kuwa kinara wa mauaji ya kimbari mwaka 1994? Tom Ndahiro anazungumza nasi akiwa mjini Kigali Rwanda.
Hayo yakijiri mkutano wa pili wa kimataifa juu ya utawala na demokrasia barani Afrika, Asia na Mashariki ya kati ulianza jana mjini Kigali nchini Rwanda.
Mkutano huo umekuja huku demokrasia na utawala bora katika nchi zinazoendelea vikikumbwa na changamoto kedekede.