Pata taarifa kuu
UFARANSA-Sheria

Ufaransa: Nicolas Sarkozy chini ya ulinzi

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozyamewekwa chini ya ulinzi , baada ya kurejeshwa nyumbani kwake akitokea kusikilizwa kwenye makao makuu ya polisi katika mji wa Nanterre. Anakabiliwa na tuhuma za kufanya ushawishi kuhusu kesi inayochunguzwa ya matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi uliopita.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy awekwa chini ya ulinzi
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy awekwa chini ya ulinzi REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa Ufaransa aliwasili chini ya ya ulinzi mkali katika makao makuu ya polisi saa mili asubuhi sa za Ufaransa sawa na saa tatu asubuhi saa za Afrika ya mashariki. Nicolas Sarkozy anachunguzwa baada ya faili ya tuhuma zinazomkabili kufunguliwa Februari 26 mwaka 2014. Kwa mujibu wa chanzo cha sheria, uamzi wa kuwaweka chini ya ulinzi mwanasheria wa rais huyo wa Ufaransa, Thierry Herzog, mmoja wa majaji waandamizi katika mahakama ya rufaa, Gilbert Azibert pamoja na jaji Patrick Sassout, ambao walisikilizwa jana, umeongezwa hadi masaa 24 yajayo.

Afisa wa kitengo cha polisi kinachopambana na rushwa ameanzisha uchunguzi ili kujua iwapo rais huyo wa zamani wa Ufaransa alijaribu kupata habari kinyume cha sheria kuhusu faili iliyobatizwa Bettencourt-Tapie/ Crédit Lyonnais, ambamo jina lake limetajwa, akiahidi kumpa wadhifa muhimu wakili wa Korti kuu Thierry Azibert, huku Sassout ambae amekua akifanya kazi moja na Thierry Azibert katika kitengo cha makosa ya jinai kwenye Korti kuu angeliteuliwa kuwa jasusi wake.

Azibert aliwahi kuendesha uchunguzi kabla, kuhusu uwezekano wa vyombo vya sheria katika mpango wa Nicolas Sarkozy kuhusu faili iliyobatizwa Bettencourt. Mawakili hao wanahusishwa pia katika kashfa nyingine ya pesa ziliyotolewa na serikali ya rais wa zamani wa Libya Moamar al Kaddafi kwa kufadhili kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2007 ya rais huyo wa zamani wa Ufaransa, baada ya mawasiliano yao kurikodiwa.

Ni kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa, rais wa zamani kuwekwa chini ya ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.