Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-Diplomasia

Ufaransa : François Hollande ziarani Afrika

Rais wa Ufaransa, François Hollande, ataanza alhamisi wiki hii ziara ya siku tatu barani Afrika, hususan katika matiafa ya Côte d'Ivoire, Niger na Chad.

Rais wa Ufaransa, François Hollande ameanza ziara ya siku 3 barani Afrika.
Rais wa Ufaransa, François Hollande ameanza ziara ya siku 3 barani Afrika. REUTERS/Thibault Camus/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya rais Hollande na viongozi hao wa mataifa matatu ya Afrika yatagubikwa na suala la usalama, wakati ambapo Ufaransa uko mbioni kuanzisha operesheni mpya inayotambuliwa kwa jina la “Barkhane” katika hali ya kupambana dhidi ya ugaidi katika maeneo ya Sahel.

Baada ya Abidjan na Niamey, rais wa Ufaransa atakua katika mji mkuu wa Côte d'Ivoiren N'Djamena jumamosi wiki hii, ambako yatawekwa makao makuu ya kikosi hicho cha kudumu chenye wanajeshi 3000 kitakacho pambana dhidi ya ugaidi.

Rais wa Ufaransa, François Hollande
Rais wa Ufaransa, François Hollande REUTERS/Philippe Wojazer

Rais Hollande anapendelea aone kwa macho yake jinsi gani kikosi hicho ambacho kimechukua na fasi ya kikosi kiliyotangulia “Serval”, ambacho kilianzishwa Januari 11 mwaka 2011 dhidi ya makundi ya wanamgambo wa kislamu wenye silaha nchini Mali kitakavyoanzisha harakati zake, washirika wa karibu wa rais Hollande wamethibitisha.

Kwa ushirikiano na nchi tano (Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger pamoja na Chad), Ufaransa umeapa kupambana na makundi hayo ya wanamgambo wa kislamu.

Duru kutoka kwa washirika wa karibu wa rais wa Chad Idrss Déby, ziara ya rais Hollande nchini Chad inatazamwa kama uungwaji mkono wa Ufaransa kwa jitihada zinazoendeshwa na Chad katika nchi za Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, na huenda rais Hollande akathibitisha kwa mara nyingine tena ushirikiano mzuri kati ya Chad na Ufaransa, zimeendelea kusema duru hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.