Pata taarifa kuu
UNHCR-Wahamiaji haramu-Usalama

UNHC yaomba mataifa ya Ulaya kutafutia ufumbuzi tatizo la wahamiaji haramu

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR limetoa tangazo, ambamo linaomba Umoja wa Ulaya kutoa msimamo wake haraka iwezekanavyo kufuatia ongezeko la idadi ya wahamiaji haramu wanaongia barani Ulaya wakipitia kwenye bahari Mediterranean.

Kamishana mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres (kulia) akiwatembelea watoto wa familia 19 000 kutoka Syria ziliyokimbilia Beyrut, Libanon..
Kamishana mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres (kulia) akiwatembelea watoto wa familia 19 000 kutoka Syria ziliyokimbilia Beyrut, Libanon.. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Katika siku 10 za hivi karibuni, zaidi ya wahamiaji haramu 260 wamefariki, na kutimiza idadi ya vifo zaidi ya 800 vya wahamiaji haramu mwaka huu.

“Vifo vya watu 260 mnamo siku zisiyozidi 10, ambao waliuawa katika mazingira ya kutatanisha, vinaonesha kuwa mzozo katika Mediterranean unaendelea kushika kasi, kamishna mkuu wa UNHCR”, Antonio Guterres amesema katika tangazo liliyotolewa na shirika hilo.

Guterres ameutaka Umoja wa Ulaya kutoa msimamo wake haraka iwezekanavyo ili kuzuia hali hiyo isiendeleyi zaidi hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Guterres ameziomba serikali za mataifa ya Ulaya kuzidisha juhudi katika shughuli zao za uokozi, na kurahisisha haraka iwezekanavyo mchakato wa kuwapa hifadhi wale wanaokimbia mataifa yao kwa kuhofia usalama wao.

Amependekeza pia kuwa mataifa hayo ya Ulaya yaandaye mazingira mazuri ya mapokezi kwa watu wanayoyakimbia mataifa yao na kutathmini kwa makini chanzo cha hali hiyo na kupatia suluhu.

Idadi hii ya vifo vya wahamiaji haramu 800 ni kubwa ikilinganishwa na vile viliyotokea mwaka 2013, ambavyo vilikua 600 na mwaka 2012 (vfo 500).

Kwa muda wa wiki moja Italia, Ugiriki, Uhispania na Malta ziliwapokea wahamiaji haramu 75.000, ikilinganishwa na mwaka 2013, ambapo walikua 60.000, huku wahamiaji haramu 22.000 wakiwa waliingia barani Ulaya mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.