Pata taarifa kuu
CAMEROON-BOKO HARAM-Usalama

Cameroon : mashambulizi ya Boko Haram yasababisha vifo

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameendesha shambulio jana jumapili katika mji wa Kolofota, kaskazini mwa Cameroon, na kusababisha vifo vya watu 16. Kwa mujibu wa idadi iliyotolewa jana jumapili, mateka wengi, akiwemo mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali, wameachiwa huru katika mazingira ambayo hayajajulikana.

Mwanajeshi wa Cameroon, lwakati jeshi likipiga doria, kaskazini mwa Cameroon.
Mwanajeshi wa Cameroon, lwakati jeshi likipiga doria, kaskazini mwa Cameroon. AFP PHOTO / REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Mateka hao ambao ni raia wa Cameroon, wametekwa nyara tangu asubuhi, baada ya shambulio hilo.

Mashambulizi mawili mfululizo kaskazini mwa Cameroon, yamezua hofu katika mji huo wa Kolofota. Watu wenye silaha wameshambulia makaazi ya kiongozi wa mji huo, Seiny Boukar Lamine, pamoja na makaazi ya naibu waziri mkuu, Amadou Ali. Askari polisi wengi, mkuu wa manispa ya jiji la Kolofota, mkewe na wasichana wake wawili, pamoja na mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali.

Kwa sasa mji wa Kolofota uko katika msiba. Watu 16 wameuawa, kwa mujibu wa idadi ya mwisho iliyotolewa jana jumapili jioni. Baadhi walichinjwa, na wengine hawakuweza kutambuliwa baada ya miili kuonekana kuwa imeharibika baada ya kurushiwa mabomu.

Katika tangazo liliyotumwa kwenye vyombo vya habari, waziri wa mawasiliano, akiwa pia msemaji wa serikali, amelani mashambulizi hayo na kuyataja kua ni ya kikatili, huku akibaini kwamba serikali imeapa kutokomeza kundi la Boko Haram.

Kundi la Boko Haram, likiwa na kiongozi wake Abubakar Shekau (katikati).
Kundi la Boko Haram, likiwa na kiongozi wake Abubakar Shekau (katikati). AFP PHOTO / BOKO HARAM

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi,”raia 4 na askari polisi wawili wameuawa” katika mashambulizi yaliyoendeshwa na watu wanaosadikiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram, ambapo baadhi ya magari yameibiwa na wapiganaji hao.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ndege za kivita za jeshi la Cameroon zimetumiwa ili kuzima mashambulizi mashambulizi hayo ya Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.