Libya : wapiganaji waendelea kudhibiti kambi za kijeshi
Kambi kuu ya kikosi maalum jijini Benghazi nchini Libya imedhibitiwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu baada ya siku kadhaa za makabiliano mashariki mwa Libya, maafisa wamethibitisha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kutokana na hali hiyo, Ufaransa inapanga kwa namna yoyote kuwaondoa raia wake nchini Libya kupitia njia ya majini, baada ya uamzi uliyochukuliwa na mataifa ya magharibi ikiwemo Marekani, Uholanzi, Canada na Bulgaria, ya kuwaondoa maafisa wa balozi zao nchini Libya.
Mataifa mengi yamewataka raia wao kuondoka chini Libya, ambako kunashuhudiwa mapigano tangu wiki mbili zilizopita kati ya makundi ya wapiganaji katika mji ya Tripoli na Benghazi.
Chanzo cha kijeshi , kimefahamisha kwamba kwamba kambi hiyo kuu ya kikosi maalum imedhibitiwa tangu jumanne wiki hii jioni na makundi ya wapiganaji wa kislamu likiwemo kundi la Ansar Asharia, ambalo liliwekwa na Washington kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.
Kundi la Ansar Asharia limeweka picha za wapiganaji wake na silaha walizokamata kwenye ukurasa wake wa facebook.
Libya inakabiliwa na hali ya kukosekana kwa utulivu tangu mapiganao ya 2011 yaliyomtimua madarakani rais Moamar Al Kadhafi, huku baadhi ya maeneo ya nchi yakidhibitiwa na wanamgambo.
Afisa wa Vikosi Maalum vya libya, Fadel al-Hassi Amewaambia waandishi wa habari jana jumanne kuwa wamejiondoa katika kambi ya kijeshi ya Benghazi baada ya mashambulizi makali ya makombora.