Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-LRA-Usalama

CAR: Kundi la LRA lanyooshewa kidole kwa kutekeleza maovu mbalimbali

Kundi la waasi wa Uganda wa Lord Resistance Army (LRA) linalopatikana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati linaripotiwa kuanzisha vitendo vya ugaidi kusini mwa nchi hiyo kwa ushirikiano na baadhi ya waasi wa zamani wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda (LRA).
Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda (LRA). AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Marekani ya “Invisible Children”, licha ya uchache wao, waasi hao wa Uganda wanatekeleza kila wiki vitendo vya kuvamia vijiji kwa malengo ya uporaji, ubakaji, mauaji na kuwateka watu.

Maeneo yaliyokua yakishambuliwa na kundi la waasi wa Uganda la LRA katika miezi kadhaa ya mwaka 2011.
Maeneo yaliyokua yakishambuliwa na kundi la waasi wa Uganda la LRA katika miezi kadhaa ya mwaka 2011. © RFI

Kiongozi wa waasi hao, Joseph Kony ambaye anatafutwa kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ya (ICC) amewaseti waasi wake katika makundi madogomadogo ya wapiganaji watano hadi 10, katika mkoa wa Haut-Mbomou ambapo wanawindwa na jeshi la Uganda pamoja na wataalam wa kijeshi wa Marekani wapatao mia moja.

William Cailleaux, mratibu wa taasisi ya Invisible Children Amesema baada ya kusambaratishwa na kukabiliwa na hali duni ya maisha misituni pamoja na vita, idadi ya waasi hao inakadiriwa kuwa ya watu kati 180 na 220 bila kuwahesabu mateka wao, wabeba mizigo na wapishi.

Uasi wa LRA umeanzishwa mwaka 1986 kaskazini mwa Uganda ambapo waasi hao wamedai kupigana dhidi ya serikali ya rais Yoweri Museveni, na baada ya mazungumzo ya amani ya mwaka 2006 kugonga mwamba, waasi hao walikimbilia kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi mwezi Machi mwaka 2008 walipoamua kupiga kambi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.