Pata taarifa kuu
Afrika Magharibi

MSF:Janga la Ebola huenda likachukua miezi 6 kudhibitiwa

Janga la Ebola ambalo linazidi kuenea kwa kasi zaidi kuliko ambavyo mamlaka zinaweza kulishughulikia linaweza kuchukua muda wa miezi sita kudhibitiwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF limesema.

Hili ni eneo lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola nchini DRC mwaka 2009.
Hili ni eneo lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola nchini DRC mwaka 2009. Luis Encinas/MSF
Matangazo ya kibiashara

Onyo hilo linakuja siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani WHO kusema kuwa kiwango cha janga hilo kilikadiliwa chini zaidi kuliko hali ilivyo na kwamba hatua zaidi ya kawaida zinahitajika kuzuia ugonjwa huo unaoua kwa kasi.

Takwimu mpya zilizotolewa na shirika la duniani WHO zinaonesha kuwa vifo vilivyotokana na ugonjwa wa Ebola kwa sasa imeongezeka na kufikia watu 1145 katika mataifa manne ya Afrika Magharibi ambayo ni Guinea, Liberia, Nigeria na Sierra Leone.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.