Pata taarifa kuu
DRC-Siasa

DRC : mvutano waendelea kati ya wanasiasa kuhusu marekebisho ya katiba

Chama cha MSR cha pili kwa ukubwa kati ya vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila kimeomba kuwepo na mjadala wa ndani ya muungano wa vyama hivyo kuamua ikiwa kuna umuhimu wa kubadili katiba kuelekea uchaguzi wa mwaka 2016.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Chama hicho kimeomba kuitishwa kwa mkutano huo, ambapo rais Kabila atashirikishwa kulingana na makubaliano ya mwishoni mwa juma lililopita baina yake na mratibu wa muungano wa vyama tawala na spika wa Bunge Aubin Minaku.

Tayari siku za nyuma, chama cha MSR kimewahi kuonyesha msimamo wake kupinga mabadiliko yoyote ya katiba kwa siri au kwa utashi wa amri ya rais au kwa amri ya mawaziri, au kikundi kingine chochote cha kisiasa bila ya mjadala wa kina.

Kwa mujibu wa vyanzo vinavyoaminika, moja ya matokeo ya mkutano huo wa mwishoni mwa juma lililopita ni pamoja na kukubaliana kuitishwa kwa mkutano huo ndani ya siku chache zijazo katika ngazi za juu za vyama hivyo.

Hatua nyingine iliyofikiwa ni kwamba mkutano huo utapaswa kuongozwa na rais Joseph Kabila mwenyewe ambapo kwa maoni ya wengi rais huyo atakuwa na fursa ya kuweka wazi msimamo wake juu ya suala la marekebisho ya katiba kuepuka kuliacha taifa kuelekea pabaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.