Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-BUNGE-Sheria-Siasa

Afrika Kusini: Julius Malema akabiliwa na adhabu kali

Bunge la Afrika Kusini linajadili taratibu za kikanuni kumsimamisha kwa muda m'bunge wa Upinzani wa chama cha EFF Julius Malema kwa tuhuma za kumshambulia kwa maneno rais wa nchi hiyo Jacob Zuma juma lililopita akijibu maswali ya papo kwa papo.

Julius Malema, m'bunge wa Upinzani wa chama cha EFF.
Julius Malema, m'bunge wa Upinzani wa chama cha EFF. REUTERS/Peter Andrews
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo ambalo serikali ya Afrika kusini pamoja na chama tawala cha ANC vinalizungumzia kuwa utovu wa nidhamu na kumkashifu rais huenda likasababisha mvutano wa kisiasa ikiwa Bunge hilo litamchukulia hatua za kinidhamu Julius Malema pamoja na wabunge wa chama chake ishirini na watano, jambo ambalo litajitokeza kwa mara ya kwanza katika miaka 20 ya demokrasia nchini Afrika Kusini.

Spika wa Bunge, Baleka Mbete, ambaye ni mtu wa karibu wa rais Zuma na mwanachama wa chama cha ANC amedhamiria kutoa adhabu baada ya uchunguzi unaoendeshwa na kamati maalum aliyoiunda ili kukomesha utovu wa nidhamu Bungeni.

Tayari watu wa karibu na rais Zuma wameanza harakati za kuunga mkono hatua hiyo, ikiwemo chama chake ambacho kimeomba Malema apewe adhabu kali, huku Umoja wa vijana wa chama hicho ukidhamiria kutumia nguvu kuitetea demokrasia dhidi ya vurugu na Chama cha Kikomunisti kikizungumzia sakata hilo kuwa kansa hatari.

Hivi majuzi, Waziri wa ulinzi, Nosiviwe Mapisa-Nqaku amenukuliwa akisema kuwa tukio hilo ni tishio kwa usalama wa wabunge na muhimili huyo, na kuomba kuhalalishwa kwa matumizi ya polisi wa kutuliza ghasia kuliokoa bunge na kuzuia machafuko yasijitokeze.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.