Pata taarifa kuu
DRC-Siasa

DRC: marekebisho ya Katiba, vyama vinavyounga mkono chama tawala vyagawanyika

Suala la kuifanyia matekebisho Katiba ya nchi kabla ya mwaka 2016 limezua wasiwasi na kuvigawa vyama vinavyounga mkono chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo cha PPRD.

AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Marekebisho hayo huenda yakampa nafasi Joseph Kabila kugombea kwenye kiti cha urais. Hali hiyo imesababisha mgawanyiko katika vyama vinavyounga mkono chama tawala, na baadhi ya vyama hivyo kupoteza msimamo.

Chama tawala na baadhi ya vyama washirika vinaunga mkono Katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho hasa kipengele cha 220 ambacho hakiruhusu rais kujichagulisha zaidi ya mihula miwili kwenye kiti hicho cha urais.

Raia wataombwa kupiga kura ya kukubali au kupinga Katiba kufanyiwa marekebisho. Hata hivo, kwa mujibu wa wadadisi, chama tawala na baadhi ya washirika wake vikiungwa mkono na baadhi ya vyama vya upinzani ambayo vilikubali hivi karibuni kushiriki katika serikali ya umoja, vimetumia mbinu hiyo ili Joseph Kabila aweze kugombea katika muhula watatu. Serikali hiyo ya umoja inasubiriwa kuundwa ifikapo Septemba 15.

Baadhi ya wajumbe wa vyama viavyounga mkono chama tawala, ambavyo havikubaliani na hoja hiyo ya chama tawala ya kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi, vimebaini kwamba vitaendelea na msimamo wao kupinga chochote kile ambacho kinaweza kudhorotesha usalama wa taifa. “Tutaendelea kuonesha msimamo wetu ili mpango huo usitekelezwi kwa maslahi ya taifa”, amesma mmoja wa wajumbe hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.