Pata taarifa kuu
RWANDA-RDF-Usalama

Maafisa wa Rwanda washitakiwa kwa uasi

Afisa wa juu wa jeshi nchini Rwanda Kanali Tom Byabagamba na generali mstaafu Frank Rusagara, wameshitakiwa Jana Ijumaa na mahakama mjini Kigali nchini Rwanda kwa kuchochea uasi kwa kueneza uvumi.

Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) wakipelekwa mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda.
Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) wakipelekwa mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda. RFI/Bryson Bichwa
Matangazo ya kibiashara

Jaji Chance Ndagano amesema kuwa maafisa hao wanashitakiwa kwa kueneza uvumi na kutishia usalama wa taifa ambapo jenerali mstaafu Rusagara anashitakiwa pia kwa kumiliki silaha.

Kanali Tom Byabagamba ambaye aliwahi kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais Kagame, alikamatwa juma lililopita siku chache tu baada ya kurejea kutoka nchini Sudani alikokuwa amekwenda katika operesheni ya kurejesha amani katika taifa hilo lenye mzozo.

Wawili hao ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wanaotuhumiwa kuukosoa utawala wa rais paul Kagame katika mfululizo wa kukamatwa kwa maafisa wa jeshi hivi karibuni.

Hayo yanajiri wakati mahakama moja nchini Afrika Kusini,kuwakuta na hatia watuhumiwa wanne kati ya sita waliokuwa wanashitakiwa kwa makosa ya kuhusika kwenye tukio la kumfyatulia risasi jenerali wa zamani wa jeshi la Rwanda,Faustine Kayumba Nyamwasa.

Faustine Kayumba Nyamwasa alikimbia nchini Rwanda na kwenda kuishi uhamishoni nchini Afrika Kusini mwaka 2010 kufuatia kuandamwa na watu anaodai wanatumwa na serikali ya rais Paul Kagame, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha vikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.