Pata taarifa kuu
EBOLA-LIBERIA-NIGERIA-UNSC-UN-Afya

Ebola: Liberia yailalamikia Umoja wa Mataifa

Viongozi wa Liberia wameamua kujitokeza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne wiki hii, ili kuhakikishia taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa wameshindwa kuidhibiti Homa ya Ebola, wakati ambapo Umoja wa Mataifa ukiahidi kuongeza juhudi za kimataifa ili kuzuia virusi hivyo.

Wakaazi wa eneo la Westpoint nchini Liberia wakiendelea kuwekwa karantini.
Wakaazi wa eneo la Westpoint nchini Liberia wakiendelea kuwekwa karantini. REUTERS/2Tango
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Liberia, Brownie Samoukai, amelitolea wito Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati, ili kuzuia ugonjwa huo wa Ebola, akibaini kwamba Ebola imekua ni tishio kwa usalama wa taifa la Liberia.

“Usalama wa Liberia uko hatarini kutokana na ugonjewa wa Ebola, ambao umekua ukisababisha vifo vya watu, na kuendelea kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi, ukiwemo mji mkuu wa Liberia, Monrovia”, amesema waziri Brownie Samoukai.

Wakati hayo yakijiri, Umoja wa Afrika AU umesema kuwa unatuma timu kadhaa za wataalamu wa kitiba magharibi mwa Afrika kwa minajili ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Shirika la habari la APress limeripoti kutoka Addis Ababa kuwa, Umoja wa Afrika unataraji kutuma wataalamu zaidi wa kitiba katika nchi zilizoathiriwa na homa ya virusi vya Ebola magharibi mwa Afrika  kwa muda wa miezi sita.

Nchi ambazo zimeathirika zaidi na mlipuko wa homa ya Ebola zinahitaji zaidi uangalizi wa kitiba ili kuweza kukabiliana na janga hilo. Umoja wa Afrika unataraji kutuma watu 100 ambao miongoni mwao watakuwemo madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine wa huduma za kitiba ili kuunga mkono jitihada zinazotekelezwa sasa ili kuzuia kuenea kwa  homa ya Ebola.

Homa hiyo ya Ebola inaonekana kuwa na nguvu zaidi tangu ilipogundulika mwaka 1976, na imekua vigumu kuidhibiti. Homa hiyo imesababisha vifo vya watu 2296 huku watu 4293 wakiwa wameambukizwa virusi vya Ebola. Nchini Liberia pekee watu 1224 wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa Ebola, Shirika la Afya Duniani WHO, limethibitisha.

Wakati huo huo vifo vya watu saba vimeorodheshwa nchini Nigeria, taifa linalostawi kiuchumi barani Afrika.

Hata hivo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, ambako kunaripotiwa aina nyingine ya Homa ya Ebola tofauti na ile inayoshuhudiwa Afrika ya magharibi, imeordhesha vifo vya watu 32 ambao wamefariki kutokana na Homa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.