Nigeria: polisi yaanzisha zoezi la kuwatafuta askari polisi 20 waliotoweka
Askari polisi ishirini wametoweka kwa kipindi cha majuma matatu sasa baada ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram kushambulia kituo cha mafunzo nje kidogo ya jiji eneo la kaskazini mwa Mji wa Gwoza. afisa mkuu wa Polisi amethibitisha.
Imechapishwa:
Hata hivyo Inspekta mkuu wa Polisi nchini Nigeria, général Suleiman Abba amewaambia wandishi wa habari kuwa polisi imeendelea na uchunguzi kubaini maeneo gani waliko.
Wakati hayo yanaarifiwa namna hiyo mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa makabiliano makali na wapiganaji hao wa kiislamu Boko Haram.
Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.
Mashahidi wamesema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, huku wanajeshi wakiondoka kwenye kambi zao. Inaarifiwa kuwa chuo kikuu katika jimbo hilo kimefungwa.