Pata taarifa kuu
DRC-CENCO-Katiba-Siasa

DRC: Cenco yapinga jaribio la marekebisho ya baadhi ya Ibara za Katiba

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inapinga marekebisho yoyote ya Ibara ya 220 ya Katiba ya nchi hiyo kulenga mabadiliko ya mihula miwili ya rais kama inavyoandikwa katika katiba ya Congo.

Baraza kuu la maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Cenco limejiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano nchini DRC.
Baraza kuu la maaskofu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Cenco limejiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano nchini DRC. cenco.cd
Matangazo ya kibiashara

Katika waraka wa maaskofu wenye jina la "kulinda taifa" na uliosomwa mbele ya vyombo vya habari, Baraza kuu la maaskofu wa Congo wanaonya kuwa jaribio lolote la kubadilisha ibara hiyo ni kupiga hatua nyuma katika jitihada za kuimarisha demokrasia na kuhatarisha mustakbali wa nchi.

Baraza kuu la maaskofu nchini Congo (Cenco) yapinga jaribio la marekebisho ya baadhi ya Ibara ya Katiba
Baraza kuu la maaskofu nchini Congo (Cenco) yapinga jaribio la marekebisho ya baadhi ya Ibara ya Katiba cenco.cd

Aidha, sambamba na kauli hiyo, maaskofu hao wameamua kujiondoa kwenye Kamati ya uadilifu na maridhiano inayofanya kazi bega kwa bega na Tume ya uchaguzi, kama ishara nyingine kwamba Kanisa Katoliki halitaki kuidhinisha mchakato wa uchaguzi ambao uko kinyume na sheria za nchi.

Kwa upande wake, serikali ya DRC imejibu kwamba maaskafu hao wamefanya maamuzi na kutoa kauli kama na hizo kwa kujibu hoja ambazo hazijawekwa mezani.

Lambert Mende, waziri wa habari akiwa pia msemaji wa serikali ya Congo.
Lambert Mende, waziri wa habari akiwa pia msemaji wa serikali ya Congo. ©RFI/Delphine Michaud

Waziri wa mawasiliano wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akiwa pia msemaji wa serikali, Lambert Mende, amesema kutoelewa kwanini Baraza hilo la maaskofu limeharakia kuchukua uamzi wakati Ibara hiyo haijajadiliwa .

“Naendelea kusisitiza kuwa hapa tulipofikia, hakuna hatua yoyote ya kisheria au ya kitaasisi iliyoamua marekebisho ya Ibara 220. sielewi maaskofu wanahisi furaha kiasi gani kujadili hoja ambazo hajiwekwa mezani”, amesema Lambert Mende.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.