Pata taarifa kuu
RWANDA-RDF-Usalama-Haki za binadamu

Rwanda: HRW yaomba uchunguzi uanzishwe kuhusu maiti ziliyoonekana katika ziwa Rweru

Shirika la kutetea haki za binadamu la HRW linatoa wito kwa uchunguzi zaidi kufuatia ugunduzi wa miili kadhaa ya watu katika ziwa Rweru kwenye mpaka wa Rwanda na Burundi.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye serikali yake inanyooshea kidole kuwakandamiza wapinzani.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye serikali yake inanyooshea kidole kuwakandamiza wapinzani. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa na RFI kutoka pande zote mbili za mpaka wa Rwanda na Burundi umebaini kuwa miili hiyo imetupwa ndani ya mto Akagera, kulingana na wakazi wa pembezoni mwa mto huo nchini Rwanda.

Msemaji wa polisi nchini Rwanda amebaini kuwa hakuna haja ya kufanya uchunguzi kwa sababu hamna mtu yeyote aliyetoweka nchini Rwanda, kauli ambayo inakanushwa na watafiti wa shirika la Human Rights Watch.

Carine Tersakian ambaye ni mmoja wa wataifiti hao wa HRW, amebaini kwamba baadhi ya familia zimewakosa ndugu zao ambao walikua wakizuiliwa katika jela mbalimbali nchini Rwanda.

“ Human Rigts Watch imebaini kuwepo kwa kutoweka kwa watu kadhaa hasa tangu mwezi Mach mwaka 2014 kaskazini-mashariki mwa Rwanda, baadhi yao wameonekana wakiwa kifungoni jela baada ya majuma au miezi kadhaa lakini wengine hawajulikani waliko, bila ya familia zao kujua waliko. Kwa kweli hakuna taarifa yoyote kuhusiana na hili na ndio maana kuna umuhimu wa kuanzisha uchunguzi”, amesema Tersakian.

Hayao yakijiri Wizara ya Sheria nchini Rwanda imechapisha orodha ya maafisa wa serikali wapatao 300 wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma na kutakiwa kurejesha fedha hizo.

Nchi ya Rwanda inakabiliwa na vikwazo ambapo misaada kadhaa ya kimataifa kutoka kwa nchi wahisani imesimamishwa miezi kadhaa iliyopita na fedha zinatakiwa kuziba ombwe huo.

Itakumbukwa kuwa juma lililopita polisi nchini humo ilitangaza kukamatwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa mfuko wa Jamii kwa usimamizi mbovu, uamuzi uliolalamikiwa na wengi wa wanaoikosoa serikali ya Kigali.

Mkurugenzi katika Wizara ya Sheria nchini Rwanda, Pierre Celestin Bumbakare, amesema wameanza sakata hilo ili kukabiliana na kashfa hiyo..

“ Tunachotaka ni watu hawa warejeshe fedha hizo serikali bila ya kusubiria hatua za kisheria, lakini pia sababu ya pili ni kwamba watu wengi hawajulikani waliko, ndio maana tunatangaza orodha hiyo ili watu watuambie ikiwa wanafahamu waliko watu hao”, amesema Bumbakare.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.