Pata taarifa kuu
EBOLA-MSF-LIBERIA-GUINEA-SIERRA LEONE-UNSC

Ebola: jumuiya ya kimataifa yaendelea kutiwa hofu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika kikao chake cha dharura chenye lengo la kuhimiza raia duniani kote dhidi ya virus vya Ebola, limetangaza kwamba mlipuko wa Homa ya Ebola, ni “tishio kwa amani na usalama wa kimataifa”.

Madaktari na wauguzi wakiva mavazi ya kuwalinda na maambukizi ya virusi vya Ebola kabla ya kumfanyia vipimo mgonjwa anaeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Sierra Leone.
Madaktari na wauguzi wakiva mavazi ya kuwalinda na maambukizi ya virusi vya Ebola kabla ya kumfanyia vipimo mgonjwa anaeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Sierra Leone. REUTERS/Tommy Trenchard
Matangazo ya kibiashara

Mchakato kuhusu azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya virusi vya Ebola umepiga hatu, licha ya kuongezeka kwa idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo.

Ni kwa mara ya kwanza azimio hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya Ebola linaungwa mkono kwa idadi kubwa ya mataifa na mashirika mbalimbali ya kihisani: nchi 134 zimependekeza majina yao yaorodheshwe.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia jitihada za Marekani, limetaka kunesha kwa jinsi gani Homa ya Ebola imekua ni tishio kwa ulimwengu. Daktari mmoja wa shirika la madaktari wasio na mipaka Msf akiwa mjini Monrovia, ametoa usahahidi ya hali inavyo endelea nchini Liberia kufuatia mlipuko huo wa Homa ya Ebola.

“ Kwa wakati huu nikiwa nazungumza, wagonjwa wamekaa mbele ya milango ya ofisi zetu, wakiomba tuwasaidie. Tunahitaji vituo vingi vya huduma za afya ili wagonjwa waweze kupata vitanda, kuliko kuendelea kusalia makwao na kuambukiza wengine”, amesema dakari huyo.

Mbali na vifo hivyo vinavyosababishwa na virusi ya Ebola, Umoja wa Mataifa umefahamisha kwamba utatuma tume maalumu mfano wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa Afrika Magharibi ili kukabiliana na Homa ya ebola hasa kusambaza msaada na kushiri katika ujenzi wa hospitali katika nchi za Liberia, Guinea aidha Sierra Leone.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa amebaini kwamba jitihada za kimataifa dhidi ya virusi vya Ebola zinapaswa kuongezeka mara ishirini ili kuhakikisha kuwa virusi hivyo vimedhibitiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.