Pata taarifa kuu
ICC-CAR-SELEKA-ANTIBALAKA-Sheria-Haki za binadam

CAR: ICC yaanzisha uchunguzi kuhusu uhalifu uliyotekelezwa tangu 2012

Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC, Fatou Ben Souda ametangaza kuzindua rasmi uchunguzi wa uhalifu uliofanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2012.

Mahakama ya Kimataifa imeamua kuazisha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadam Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mahakama ya Kimataifa imeamua kuazisha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadam Jamhuri ya Afrika ya Kati. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Fatou Ben Souda amesema kuwa tayari ofisi yake imekusanya taarifa ambazo zinabaini makundi ya Seleka na Anti- Balaka kuhusika katika vitendo vya ukatili dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Tangu mwezi Februari mwendesha mashitaka wa mahakama ya Kimataifa alichukua uamzi wa kuanzisha uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Jamhuri ya Afrika ya Kati, Fatou Bensouda alianzisha uchunguzi wa mwanzo na kubaini kuwa Mahakama ya Kimataifa ICC kinayo majukumu ya kushughulikia visa vya ukiukwaji wa haki za binadam viliyoshuhudiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2014.

Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa imethibitisha kwamba ina vithibitisho vya mwanzo ambavyo vinaonesha kwamba kundi la waasi wa zamani wa Seleka na wanamgambo wa kikristo wa Anti-balaka walitekeleza uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za binadam.

Mwishoni mwa mwezi Mei, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza alichukua uamzi wa kuwasilisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ripoti ihusuo ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mahakama ya Kimataifa imeazisha uchunguzi ili kuwatambuwa waliyohusika na uhalifu ili waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.