Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-Utekaji nyara

Hervé Gourdel auawa: wahalifu waendelea kutafutwa Algeria

Baada ya tangazo la kuuawa mateka wa Ufaransa Hervé Gourdel, alietekwa nyara jumapili nchini Algeria na kundi lenye mafungamano na wapiganaji wa Dola la Kiislam IS, serikali ya Algiers imelani kitendo hicho na kubaini itahakikisha imewakamata wahalifu.

Msafara wa wanajeshi wa Algeria karibu na kijiji cha Ait Ouabane katika jimbo la Kabylie, ambako Hervé Gourdel aliuliwa.
Msafara wa wanajeshi wa Algeria karibu na kijiji cha Ait Ouabane katika jimbo la Kabylie, ambako Hervé Gourdel aliuliwa. EUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Algiers imetuma salamu za rambi rambi rasmi kwa familia ya raia huyo wa Ufaransa na viongozi wa Ufaransa. Tangazo hilo la serikali ya Algeria limesomwa jumatatu wiki hii na mwanahabari wa Algeria aliekua akitangaza habari.

Waziri wa Ulinzi wa Algeria ametoa tangazo akithibitisha kwamba nyenzo malimbali ziliwekwa ilikuhakikisha kuwa mateka huyo mwenye umri wa miaka 55 anapatikana bila hata hivo mafanikio.. Operesheni hiyo ilikuaikiendeshwa na kikosi cha wanajeshi 2000. kwa mujibu wa vyanzo vya usalama operesheni hiyo bado inaendelea ili kuwadhibiti wahalifu hao.

Muungano wa mashirika ya kiraia nchini Algeria pamoja na chama chenye wafuasi wengi katika jimbo la Kabylie RCD vimelani kitendo hicho kiovu dhidi ya raia wa Ufaransa, Hervé Gourdel, huku vikiikemea serikali ya Algeria kuendelea kupuuzia vitisho vya kigaidi vinavyoendelea kutolewa na makundi ya kigaidi nchini Algeria.

Maandamano ya kuomba Hervé Gourdel aachiwe huru yaliyopangwa kufanyika alhamisi wiki hii katika mji wa Tizi Ouzou yataendelea kama ilivyopangwa, lakini kwa sasa itakua si maandamano ya kuomba achiwe huru bali ya kutoa heshima za mwisho, baada ya kuuliwa kwa mateka huyo na kulani kitendo hicho cha kumuua kinyama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.