Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-LIBERIA-EBOLA-Afya

Sierra Leone: serikali yaanzisha mikakati ya kupambana na Ebola

Rais Ernest Bai Koroma amesema wilaya za Port Loko, Bombali na Moyamba ndio ziliyoathiriwa zaidi, na watu zaidi ya milioni moja wapo hatarini kuambukizwa Ebola.

Watu waliojitolea wakijiandaa kubeba muiili wa mtu aneshukiwa kufariki kutokana na Homa ya Ebola katika kijiji cha Pendebu, Julai 18 mwaka 2014, Sierra Leone.
Watu waliojitolea wakijiandaa kubeba muiili wa mtu aneshukiwa kufariki kutokana na Homa ya Ebola katika kijiji cha Pendebu, Julai 18 mwaka 2014, Sierra Leone. REUTERS/WHO/Tarik Jasarevic/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Sireleon imeamuru watu kutotoka nje katika wilaya tatu ambazo ni Porto Loko, Bombali na Moyamba katika juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola.

Uamuzi huu unakuja siku chache tu baada ya agizo lingine kama hili kumalizika kote nchini ambapo watu walilazimika kukaa nyumbani kwa muda wa siku tatu ili kupata mafunzo ya namna ya kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu.

Watu 593 wamepoteza maisha nchini humo kutokana na Ebola na wenginze zaidi ya elfu moja na mia nane kuambukizwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO.

Rais wa Marekani, Barack Obama, akitolea wito jumuiya ya kimataifa kukabiliana na virusi vya Ebola.
Rais wa Marekani, Barack Obama, akitolea wito jumuiya ya kimataifa kukabiliana na virusi vya Ebola. REUTERS/Larry Downing

Wakati huo huo rais wa Marekani Barrack Obama, amesema jumuiya ya kimataifa haifanyi vya kutosha kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola katika Mataifa ya Afrika Magharibi.

Obama amewaambia wajumbe wa Umoja wa wa Mataifa jijini New York kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya ikiwa dunia itafanikiwa kupambana na janga hilo baya kuwahi kushudiwa duniani.

Watu zaidi ya elfu mbili wamepoteza maisha nchini Liberia, Sireloen, Guinea na Nigeria na wengine zaidi ya elfu sita kuambukizwa.

Marekani, imetuma wanajeshi elfu tano katika mataugfa hayo kusaidia kupambana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa dharura kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Ebola katika ukanda wa Afrika magharibi – UN MEER, uliyoundwa na Umoja huo unatarajiwa kuanza kazi yake ya utafiti siku ya Jumapili.

Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Margaret Chan, ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano mahususi siku ya Alhamisi wiki hii kuhusu kiwango cha juu cha Ebola kubaini kuwa kunahitajika uharaka wa kiutendaji kutoka kwa jumuia ya kimataifa .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.