Pata taarifa kuu
BURUNDI - SHERIA

Mwanaharakarati mtetezi wa haki za binadamu nchini Burundi Pierre Claver Mponimpa aachiwa huru kwa dhamana

Mahakama kuu jijini Bujumbura imemuacha huru kwa dhamana mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu na wafungwa Pierre Claver Mponimpa.

Pierre Claver Mponimpa mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu nchini Burundi
Pierre Claver Mponimpa mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu nchini Burundi
Matangazo ya kibiashara

Mbonimba Ambaye ananyemelewa na maradhi ya kisukari, mawakili wake wamekuwa wakiomba mahakama hiyo kumuacha huru kwa dhamani, hatuwa ambazo hapo awali hazikufua dafu.

Mahakama hiyo imemumuru Mbonimpa kutotembea nje ya jiji Kuu la Bujumbura wakati huu akiwa huru kwa dhamana. Mbali na hayo, Mahama hiyo imemtaka kuripoti mahakamani kwa wakati wowote atapohitajika.

Upande wa mawakili watetezi wamesema kuridhishwa na hatuwa hiyo.

Pierre Mbonimpa anatuhumiwa makosa ya kuyumbisha usalama wa nchi kwa kuwasilisha ushahidi mahakamani wa uongo juu ya uwepo wa vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd "Imbonerakure" katika bonde la Rusisi eneo la DRCongo.

Mataifa kadhaa ya magharibi ikiwemo Marekani yamekuwa katika mstari wa mbele kuiomba serikali ya Burundi kumuacha huru kiongozi huyo wa shirika la Aprodh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.