Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Burundi yajadiliana na Marekani juu ya swala la FBI kushiriki katika uchunguzi wa watu waliookotwa katika ziwa Rweru

Majadiliano yanaendelea kati ya serikali za Burundi na Marekani juu ya kuanzisha uchgunguzi kuhusu miili ya watu iliookotwa hivi karibuni katika ziwa Rweru mpakani mwa Burundi na Rwanda. Miili ya watu wasiojilikana ambayo ilikuwa imefungwa kamba na kuwekwa ndani ya mifuko iliokotwa na wavuvi katika ziwa hilo.

Jopo la wataalamu wa FBI wakichukuwa viashiria
Jopo la wataalamu wa FBI wakichukuwa viashiria Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa serikali ya Burundi walichukuwa uamuzi wa kuzika miili miine ilionekana kwa mara ya kwanza bila hata hivyo kuendesha uchunguzi wa aina yoyote. Ikulu ya rais nchini Burundi ilikuwa imetaja ombi la shirika la ujasusi la Marekani FBI, kuingilia kati katika uchunguzi, bila hata hivyo kuweka bayana mbinu na njia za uingiliaji wa Marekani katika uchunguzi huo.

bandari ndogo ya ziwa Rweru Rweru, eneo ambalo ilipozikwa miili ya watu wanne iliokotwa
bandari ndogo ya ziwa Rweru Rweru, eneo ambalo ilipozikwa miili ya watu wanne iliokotwa RFI / Esdras Ndikumana

 Kile ambacho kinaweza kuthibitisha kwa sasa ni kwamba, Washington ilitowa pendekezo kwa serikali ya Burundi la kusihiriki kwenye uchunguzi wa kubaini miili hiyo, pendekezo ambalo lilipokelewa vema na Burundi. Juma lililopita Marekani ilizitolea wito serikali za Burundi na Rwanda kufanya uchunguzi wa kina hususan kubaini miili ya watu hao ni kina nani.

Marekani inasema pendekezo kama hilo lilitolewa pia kwa serikali ya Kigali, na hakuna mtazamo wowote uliotolewa na serikali hiyo, inayoona kwamba swala hilo linaihusu  Burundi pekee. Jambo ambalo serikali ya rais Nkurunziza inatupilia mbali na kusema kwamba miili hiyo imekuja katika ziwa Rweru ikitokea katika Mto kagera nchini Rwanda. Ushuhuda ulitolewa na watu mbalimbali katika eneo hilo la mpaka, umethibitisha kuwa miili hiyo imetoka katika mto Kagera.

Ziwa Rweru.
Ziwa Rweru.

Kuhusu uwezekano wa ujio wa watalaamu wa FBI jijini Bujumbura, Marekani inasema bado ni mapema kujuwa ni njia gani zitazotumiwa katika kutowa msaada. Serikali ya Burundi yao inakiri kuwa na haja ya wataalamu wa Polisi. Duru za serikali zinasema kwamba hakuna la kuficha kwa sasa na kuweka bayana kwamba majadiliano yanaendelea kubaini njia za msaada wa Marekani na Kalenda kukizingatia ombo lililotolewa na serikali ya Burundi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.