Pata taarifa kuu
RWANDA-UPINZANI-Katiba-Siasa

Rwanda: Mjadala waibuka kuhusu marekebisho ya Katiba

Mjadala umeibuka nchini Rwanda kuhusu uwezekano wa kuifanyia marekebisho Katiba ya nchi hiyo.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame. AFP PHOTO / CARL COURT
Matangazo ya kibiashara

Vyama vitatu ambavyo vinadai kuwa upande wa upinzani vimependekeza kufanyike kura ya maoni kuhusu marekebisho ya Katiba ili kumuwezesha rais Paul Kagame kugombea kwa muhula wa tatu

kulingana na Katiba ya Rwanda, rais wa Rwanda Paul Kagame hawezi kugombea muhula wa tatu, baada ya kuhitimisha muhula wake wa pili ifikapo mwaka 2017.

Tawi la chama cha PS-Imberakuri linalotambuliwa na utawala wa Rwanda ni miongoni mwa vyama hivyo vitatu vinavyopendekeza Katiba ifanyiwe marekebisho. Kwa mujibu wa kiongozi wa tawi hilo, Christine Mukabunani, rais Paul kagame amekua ni kivutio kwa raia wa Rwanda, kuna umuhimu aweze kugombea katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017 iwapo Katiba itafanyiwa marekebisho.

“ Sehemu zote rais Kagamme anapotembelea, raia wamekua wakimuomba agombeye katika uchaguzi wa mwaka 2017. Chama chetu kinatetea uwepo wa misingi ya kidemokrasia nchini Rwanda, na ndio maana tunapaswa kuwapa nafasi raia wachukuwe uamzi”, amesema Mukabunani.

Kauli hiyo imeungwa mkono na chama cha PDI cha waziri wa mambo ya ndani, Musa Fazil Harerimana. Akihojiwa na RFI, Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Rwanda amebaini kwamba chama chake kimepinga mara kadhaa kukadiriya mihula ambayo rais anatakiwa awe madarakani, akisema kwamba ni bora zaidi kuwapa nafasi raia wachukuwe uamzi. Musa Fazil Harerimana amesema akisisitiza kwamba rais Paul Kagame ni rais bora ambaye anatakiwa kuendelea kuliongoza taifa la Rwanda.

Chama kingine cha PSP, kikinukuliwa na vyombo vya habari vya Rwanda, kimeunga mkono penekezo la kuitisha kura ya maoni.

Kwa upande wake chama cha Kijani, ambacho ni chama cha mwisho kusajiliwa kwenye wizara ya mambo ya ndani, ambacho kimekua kikinyooshea kidole na utawala wa Rwanda kimepinga uwezekano wowote wa kuifanyia Katiba marekebisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.