Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: raia waukimbia mji wa Beni

Watu zaidi ya telathini wameuawa Alhamisi wiki hii mjini Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuvamiwa na waasi wa Uganda wa ADF.

Raia wa mji wa Beni wameanza kuukimbia mji huo kufuatia shambulio la waasi wa Uganda wa ADF-Nalu Ahamisi Oktoba 16 mwaka 2014, shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu zaidi ya 30.
Raia wa mji wa Beni wameanza kuukimbia mji huo kufuatia shambulio la waasi wa Uganda wa ADF-Nalu Ahamisi Oktoba 16 mwaka 2014, shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu zaidi ya 30. AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Hili ni shambulio la kipekee ambalo limegharimu maisha ya watu wengi kwa muda mfupi.

Mauaji hayo yameleta wasiwasi mkubwa katika mji huo, huku mashirika ya kiraia yakitaka serikali ya Kinshasha, na majeshi ya Umoja wa Mataifa kuendeleza operesheni ya kuwoandoa waasi hao.

Shambulio hilo pia limeziweka mashakani hotuba za viongozi wa Congo ambao mara kwa mara wamekua wakibaini kwamba kundi la waasi wa ADF limetokomezwa.

Wakati hayo yakijiri, mamia ya wakaazi wa maeneo yaliyo karibu na mji Beni wamekua wakiyahama makaazi yao, baada ya shambulio hilo. Raia wa Beni na vitongoji vyake wameingiliwa na hofu baada ya kuonekana barabarani nyaraka zinazotishia kutokea kwa shambulio jingine la waasi wa ADF kwenye uwanja wa ndege.

Kwa muda wa siku 15 watu 53 wameuawa, yameeleza mashirika ya kiraia. Tangu wiki mbili zilizopita mashambulizi yanayowalenga raia yameendeshwa katika maeneo yaliyo pembezuni mwa mji wa Beni kwenye umbali wa kilomita 70 na mpaka wa Uganda, katika maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watu wenye silaha wamekua wakiingia usiku katika maeneo hayo, wakiwaibia raia mali zao na kuaua kwa mapanga.

Naibu Mwenyekiti na msemaji wa mashirika ya kiraia mashariki mwa Congo, Omar Kavota, amesema Mahakama ya Kimataifa ICC inastahili kuingilia kati na kuchunguza mauaji haya na kuwachukulia hatua wanayoyatekeleza.

Sherehe za mazishi kwa watu hao waliouawa Alhamisi wiki hii zimepangwa kufanyika leo Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.