Pata taarifa kuu

Nigeria yafikia makubaliano na Boko Haram kuhusu kuachiliwa huru wasichana waliotekwa na kusitisha mapigano

Viongozi na wanaharakati hii leo wanasubiri kwa hamu kubwa kujua habari zaidi juu ya hatima ya zaidi ya wasichana 200 waliotekwa na kundi la Boko Haram miezi sita iliyopita baada ya serikali ya Nigeria kudai kuwa ilifikia makubaliano na Boko Haram juu ya kuachiliwa kwao.

Afisa mkuu wa ulinzi Alex Badeh alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa mapigano yamefikiwa kati ya serikali ya shirikisho ya Nigeria na kundi la Boko Haram
Afisa mkuu wa ulinzi Alex Badeh alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa mapigano yamefikiwa kati ya serikali ya shirikisho ya Nigeria na kundi la Boko Haram globalpost.com
Matangazo ya kibiashara

Afisa mkuu wa ulinzi Alex Badeh alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa mapigano yamefikiwa kati ya serikali ya shirikisho ya Nigeria na kundi la Boko Haram.

Tangazo la badeh linakuja baada ya katibu wa raisi Goodluck Jonathan Hassan Tukur kueleza kuwa makubaliano ya kukomesha vitendo vya kikatili sambamba na kuachiwa huru wasichana 219 wanaoshikiliwa mateka na kundi hilo yamefikiwa kati ya serikali na wanamgambo hao.

Tukio hili linakuja baada ya maandamano yaliyofanyika juma hili ya kudai kuachiwa kwa wasichana hao ambao walitimiza miezi sita tangu washikiliwe na Boko Haramu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.