Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF-Usalama

DRC: raia wa Beni wamekata tamaa juu ya usalama wao

Wananchi wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo DRC, hawana imani na kauli za viongozi wa eneo hilo baada ya kutokea kwa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, chini ya mkono wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF-Nalu.

Raiawa kiyahama makaazi yao wakihofia usalama wao kutokana na mshambulizi ya waasi wa Uganda wa ADF-Nalu. en prΓ©vision des combats des FARDC contre les rebelles de l'ADF-Nalu dans l'est du Congo, le 18 janvier 2014.
Raiawa kiyahama makaazi yao wakihofia usalama wao kutokana na mshambulizi ya waasi wa Uganda wa ADF-Nalu. en prΓ©vision des combats des FARDC contre les rebelles de l'ADF-Nalu dans l'est du Congo, le 18 janvier 2014. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Licha ya wito uliotolewa na Mea wa jiji la Beni Nyoni Masumbuko kuwataka kusalia kuwa watulivu katika kipindi hiki jeshi la serikali likifuatilia kwa ukaribu zaidi swala la Usalama, wananchi wengi wameendelea kuutoroka mji huo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiendesha mashambulizi dhidi ya waasi wa ADF-Nalu kwenye mpaka na Uganda.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiendesha mashambulizi dhidi ya waasi wa ADF-Nalu kwenye mpaka na Uganda. AFP/Alain Wandimoyi

Kundi la ADF-Nalu limeendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia yoyote licha ya jeshi la serikali kutangaza kuwa limewadhibiti kwa asilimia kubwa waasi hao.

Wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakihoji kuhusu uwezo wa kundi hilo kuingia hadi katika eneo ambalo lina wakaazi wengi wakiwemo wanajeshi wa serikali na kutekeleza mauaji kwa kuwakata watu kwa mapanga na kufaulu kutoroka bila wasiwasi wowote.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya DRC imetuma ujumbe wa watu wasiopungua ishirini kuchunguza mauaji yaliyotokea wilayani Beni juma lililopita.

Wakati huohuo wafungwa 400 wa jela la Butembo mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefaulu kutoroka, na kuzua mtafaruku mkubwa katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.