Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC-FDLR-CRGL-IGAD-SADC-Usalama

Rwanda: DRC: FDLR haijatekeleza ahadi zake

Uwepo wa waasi wa Kihutu wa Rwanda katika aridhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado kunaendelea kutia wasiwasi mataifa ya ukanda wa maziwa makuu.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009. AFP/ Lionel Healing
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya maendeleo ya Afrika ya Mashariki pamoja na shirikisho la mataifa ya Ukanda wa Maziwa Makuu vilikutana jumatatu wiki hii nchini Angola. Mkutano huo uligubikwa na suala la kuwapokonya silaha waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wanaoendesha harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa muda wa miaka 20 sasa.

Mwishoni mwa mwezi Mei, waasi hao waliomba kuweka silaha chini kwa hiyari yao. Mwezi Julai, baada ya kuona kuwa hakuna maendeleo yoyote katika zoezi hilo, mataifa ya ukanda wa maziwa makuu yaliwapa waasi hao muda wa ziada wa miezi sita, hadi Januri 2, ili wawe wamekwisha pokonywa silaha..

Kwa muda wa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa yoyote kuhusu zoezi la kuweka silaha chini linaloendeshwa na waasi hao. Mataifa 16 ya Ukanda wa Maziwa Makuu pamoja na mataifa ya Afrika ya Mashariki yakiungwa mkono na Jumuiya ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika wamekubaliana kutumia nguvu kwa kuwapokonya silaha waasi hao iwapo watakua hawajaweka silaha chini ifikapo Januari 2.

Kwa muda wa miezi mitatu inayosalia kabla ya kutamatika muda uliyotolewa, shirikisho la mataifa ya Ukanda wa Maziwa Makuu pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya mataifa ya Afrika ya Mashariki vimeiomba tume ya Umoja wa Matiafa nchini Congo Monusco kufanya kilicho chini ya uwezo wao kuhakikisha kuwa waasi wanao jisalimisha wanapokelea katika mazingira mazuri, jambo ambalo huenda likawaridhisha waasi hao, kwani walikua wakieleza wasiwasi wao kuhusu usalama wao watakapo jisalimisha na kukuwekwa katika makambi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.