Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SOKA-Usalama

Afrika Kusini: Nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini auawa

Nahodha na kipa wa timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini, Bafana Bafana Senzo Meyiwa ameuawa baada ya kupigwa risasi jijini Johannesburg.

Nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa mkaka 2013.
Nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa mkaka 2013. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema kuwa, Meyiwa ambaye pia alikuwa mchezaji wa klabu ya Orlando Pirates alipigwa risasi baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kuvamia nyumba ya mpenzi wake na kutekeleza mauaji hayo.

Kabla ya kuuawa kwake, Meyiwa mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu yake Jumamosi iliyopita na kuisaidia timu yake kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya kuwani taji la ligi ya soka nchini humo.

Timu ya taifa taifa ya Afrika Kusini bafana bafana.
Timu ya taifa taifa ya Afrika Kusini bafana bafana. AFP/Alexander Joe

Aidha, amekuwa nahodha kipindi chote cha mechi nne za Afrika Kusini kutafuta tiketi ya kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Morroco.

Polisi wameongeza kuwa, watu wawili waliokuwa na silaha waliingia katika makaazi ya mpenzi wake Meyiwa, na mwingine kusalia nje kabla ya kufyatua risasi.

Haijafagamika mauji hayo yalifanyika kwa nia gani, wakati huu polisi wakitoa Dola za Marekani 14,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa muhimu kusaidia kukamatwa kwa wauaji hao.

Wapenzi wa soka nchini Afrika Kusini na kwingineko dunia, wameendela kutuma risala za rambirambi kwa famlia ya mchezaji huyo ambaye katika siku za hivi karibuni amejipatia umaarufu kutokana na kuonesha kiwango cha juu cha soka katika klabu yake na timu ya taifa.

Katika michuano ya kufuzu kwenda Morroco kucheza fainali za Afrika, Meyiwa bado hajafungwa bao lolote katika michuano katika kundi lao ambalo wanongoza kwa alama 8.

Mwezi ujao, Afrika Kusini watakuwa nyumbani dhidi ya Sudan kabla ya kusafiri kwenda jijini Abuja kumenyana na Nigeria katika mchuano wa mwisho, michuano ambayo wachezaji wenzake watamkosa nahodha wao Senzo Meyiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.